Habari za Punde

MSANII ROMA MKATOLOKI AANIKA SAKATA LA KUTEKWAMsanii wa muziki wa kizazi kipya,  katika miondoko ya Hipo Hop, Ibrahim Musa 'Roma Mkatoliki' akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni ya leo,  wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake pamoja na wasanii wenzake walipokuwa katika studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki jijini Dar es salaam. Roma ameiomba Serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujumla kutoka na hali ilivyo kwasasa ambapo matukio ya kutekana yamezidi kuchukua nafasi kila kukicha. Kushoto kwake ni Waziri wa habari , Sanaa,  Utamaduni na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe.

‘Roma Mkatoliki’ akiendelea kuelezea sakata.
Roma Mkatolikií.  akionyesha makovu aliyoyapata alipokuwa ametekwa na watu wasiojulikana hivi karibuni.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo alipokuwa ajibu maswali kuhusu tukio la kutekwa kwa Msanii, Roma Mkatolikií. Wa (tatu kushoto waliokaa) ni Mke wa msanii huyo, Nancy Ibrahim Mussa. 

Msanii, Ibrahim Musa, 'Roma Mkatoliki' akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo,wakati wa mkutano huo jioni ya leo, wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake pamoja na wasanii wenzake walipokuwa katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam. Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujumla kwakuwa hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha kwa  wasanii na watanzania kwa ujumla. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.