Habari za Punde

MSIBA WA BINTI ALIYEIBUKIA MAKABURINI AKIWA HAI, WAHAMIA KWA JIRANI YAKE

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
MAUZAUZA ya msiba wa Binti aliyegongwa na gari na kufariki yamezidi kuchukua nafasi huko maeneo ya Gold Star Mbezi juu, baada ya mwili wa binti aliyetambuliwa na baadhi ya nduguze katika chumba cha kuhifadhia maiti, Hospitali ya Mwananyamala, kutambuliwa jana kuwa ni  rafiki na jirani wa Anna, aliyekutwa makaburini akiwa hai,  wanaoishi mtaa mmoja huko Mbezi Juu, Dar es Salaam.
Baada ya tukio la juzi familia ya Anna na ya marehemu Juliana Tawele (32) waliongozana na Polisi hadi Hospitali ya Mwananymala jana kwa ajili ya kuutambua mwili uliosemekena kuwa ni wa Anna na kukuta ni wa rafiki na jirani yake Anna,  aliyefahamika kwa jina la Juliana Tawele,  ambaye pia alifariki kwa kugongwa na gari tena eneo lilelile lililoelezwa kugongewa Anna na muda ule ule.
Aidha imeelezwa kuwa Hospitalini hapo Anna alichukuliwa vipimo ambavyo majibu yake hayakutolewa wala kufahamika ni vipimo gani huku, wanandugu wa Anna wakishauliwa kwenda kumhoji vizuri mtoto wao ni wapi alikokuwa tangu alipoondoka nyumbani hadi kukutwa makaburini  huku akiwa na kitambaa chekundu mdomoni na akilia bila kuongea.
Majirani wa mtaa huo bado wanaonyesha kushangazwa na mkanganyiko wa tukio hilo la aina moja la majirani hao na zaidi kuwashangaa wanandugu 1o kati ya 11 akiwamo baba mzazi walioingia chumba cha maiti na kutambua kuwa maiti waliyoiona ilikuwa ni ya mtoto wao bila kujua kuwa waliyemuona alikuwa ni mtoto wa jirani yao tena rafiki wa mtoto wao.

Aidha majirani hao waelezea mshangao wao baada ya askari waliobeba mwili wa mtu alyegongwa maeneo ya Mbezi Tangi Bovu waliofika eneo la tukio juzi na kumkuta Binti aliyedaiwa kufa na wao kushangazwa  kwa kusema kuwa sura ya binti Anna ndiyo hasa waliyoibeba katika tukio hilo la ajali.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.