Habari za Punde

MVUA ZILIVYOZUA KIZAAZAA MITAA YA DAR LEO

 Hapa ni mitaa ya Mwananyamala kwa Ali Maua....
 Nyumba zikiwa zimezingirwa na maji eneo la Kijitonyama Darajani kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, leo.
 Mpita njia akikatika katikati ya maji mitaa ya Msasani barabara ya Mwai Kibaki
 Nyumba zikiwa zimezingirwa na maji eneo la Mwananyamala kwa Ali Maua, kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, leo
 Kijana akiwa membeba mwanafunzi ambaye hakuweza kufahamika mara moja ni wa shule gani, akimvusha katika eneo lililofurika maji Mwananyamala kwa Ali Maua, kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, leo. 

Mfanyabiashara wa Maandazi na mikate, akikokota baiskeli yake iliyo na matenga matupu, kuvuka maji yaliyofurika eneo la Msasani kwa Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
 Wakazi wa Mwanayamala kwa Ali Maua wakiwa wamebarizi nje ya nyumba zao zilizozingirwa na maji
 Watoto wakiwa wamepumzika nje ya nyumba yao iliyozungukwa na maji eneo la Mwananyamala kwa Ali Maua jijini Dar es Salaam,leo.
Mkazi wa Kijitonyama Darajani, akiwa katikati ya maji  yenye kasi huku nyumba zilizo eneo hilo zikiwa zimezingirwa na maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, leo
  Mwokota Chupa chakavu ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, akining'inia darajani akijaribu kudaka chupa zilizokuwa zisukumwa na maji ya mvua katika daraja hilo lililopo Tandale kwa Mtogole, kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, leo.
 Hii siyo Swimming Pool bali ni uani kwa mtu hapa pakiwa pamejaa maji kutokana na mvua za leo.
 Mama Lishe akiwa katika eneo lake la kazi huku akiwa amezingirwa na maji kama alivyokutwa na mpiga picha eneo la Msasani kwa Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo.
 Hapa hajui afanye nini....
Anatafuta wateja......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.