Habari za Punde

MWILI WA ALIYEKUWA KIONGOZI WA FREEMASON TANZANIA, ANDY CHANDE WACHOMWA MOTO DAR LEO

 Aliyekuwa Kiongozi wa Jumuia ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, kwa miaka 40, Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy’ Chande, akiwa amebebewa na baadhi ya waombolezaji, ndugu na jamaa, kuelekea kuchomwa moto katika makaburi ya Wahindi yaliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam, leo mchana. Picha ndogo juu (kushoto) ni waombolezaji wakipeleka makaa ya moto kuanza kuwasha moto. Picha ndgo ya juu (katikati) ni moto ukiwashwa na juu (kulia) ni Mwili huo ukichomwa moto.
Picha ndogo chini (kushoto) ni Kituo cha mwisho cha marehemu ambapo akitoka nyumbani hufikishwa hapo kabla ya kuanza kuchomwa na ya (kulia chini) ni Rafiki wa marehemu, aliyejitambulishwa kwa jina la Ramesh Shaa, akihojiwa.
Mfanyabiashara maafuru nchini Jitu Patel (kulia) akiwafariji baadhi ya watoto na ndugu wa marehemu, baada ya mwili wa marehemu kuwashwa moto, leo mchana katika makaburi ya Wahindi Makumbusho.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.