Habari za Punde

MZEE MZINDAKAYA AFUNGUKA KUZUSHIWA KIFO, ASEMA ANAMWACHIA MUNGU

 Mbunge mstaafu na mwanasiasa mkongwe nchini, Chrisant Mzindakaya, akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa akikanusha habari zilizosambaa katika baadhi ya Mitandao ya Kijamii, zikimzushia kifo. Mzindakaya alisema kuwa kulingana na umri wake hana muda wa kuwafuatilia watu hao na kuwawajibisha ama kuwachukulia hatua za kisheria kwa kosa hilo, ila ameamua kumuachia mungu.
Akielezea kuhusu mshtuko baada ya habari hizo, alisema kuwa amekuwa katika wakati mgumu kwa kipindi kifupi baada ya kuenea kwa habari hizo huku akipigiwa simu na watu wengi na hata nduguze wakisumbuliwa kuhusu habari hizo.
Nilishangazwa sana na habari hizi nilipoonyeshwa na wanandugu ambao nao baadhi yao wakiwa nyumbani walishtushwa wakihisi ni habari za kweli kwani walishangaa zaidi kuniacha nikiwa na ahueni na nikiendelea vizuri lakini ghafla wakapata habari hizo.
''Kiukweli nimesikitishwa sana na wazushi hawa wasiofuata maadili ya kazi zao wala utu, muongozo wa kazi zao, ila namuachia mungu kwa hiki walichokifanya kwani inawezekana wameniongezea umri wa kuishi, kwani kwa matibabu na huduma niliyoipata katika Kituo hiki hata daktari amefarijika kwa hatua niliyofikia na amesema leo nitaruhusiwa''. alisema Mzee Mzindakaya
 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, akisalimiana na Mzee Mzindakaya, wakati alipofika Hospitalini hapo kumjulia hali na kumpa pole kutokana na habari hizo za uzushi zilizoenea. 
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, (kushoto) Crisant Mzindakaya, na Daktari Bingwa na Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo Hospitali ya Muhimbili, Peter Kisenge. wakiwa katika picha ya pamoja hospitalini hapo Muhimbili, baada ya mazungumzo na waandishi wa habari. Picha na Habari Muhidin Sufiani (MAFOTO)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.