Habari za Punde

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM (BARA) RODRICK MPOGOLO ASHIRIKI KUFANYA USAFI KWENYE SHAMBA LA CCM KIJIJI CHA MUHUWESI WILAYA YA TUNDURU MKOANI SONGEA

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo (kulia) na baadhi ya viongozi wakishiriki kufanya usafi wa mazingira, katika shamba la CCM Kijiji cha Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Songea.
**********************************
Na Mwandishi Wetu, Tunduru 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema viongozi wake waliopora na mali za Chama kwa maslahi binafsi hawakubaliki katika kipindi hiki cha mageuzi. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo alisema hayo jana alipozungumza na wanachama na viongozi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, kilichofanyika mjini hapa.
Alisema katika mabadiliko yanayofanyika sasa ni yanalenga kuiwezesha CCM inatumia rasilimali zake kujiimarisha na kujitegemea kiuchumi. 
Aliwataka viongozi na watendaji kutumia rasimali na vitega uchumi kwa maslahi ya Chama na kuhakikisha maeneo yote yanamilikiwa kisheria.
Mpogolo alisema viongozi waliouza viwanja vya Chama hawana nafasi ndani ya  Chama kwa kuwa kuna ufuatiliaji wa karibu ili mali zote zitumike kuimarisha Chama. 
Alisema katika mageuzi hayo wanachama wote wanatakiwa wabadilike waondokane na roho za ufisadi na wajenge uadilifu utakaowavutia walioko nje ya  kujiunga na CCM.
Kwa upande wake Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha), Dk. Frank Haule, alisema ili Chama kiendelee kinatakiwa kuwa na fedha katika uendeshaji wa shughuli zake. 
Alisema mataifa ya China, Marekani na Korea  ni mataifa yenye jeuri inayotokana na nguvu za fedha, hivyo kwa CCM ikijiimarisha kiuchumi kitaendelea kuwa na nguvu. 
Dk.Haule aliwataka viongozi  kujenga nidhamu na uadilifu katika kazi zao ili kuhakikisha mali zote zinasimamiwa vizuri na kunufaisha Chama. 
Awali Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Tunduru, alisema wanaishukuru serikali ya CCM kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Masasi/Tunduru /Songea.Alisema kwa sasa wanasafiri kwa saa tatu kwenda Songea na Masasi badala ya kutumia siku nzima, kabla ya kuwekwa lami. 
Mapema viongozi hao walitembelea maeneo ya Chama ikiwemo shamba lenye ukubwa wa hekta 268 katika Kijiji cha Muhuwesi na kushiriki  kufyeka nyasi kabla ya kukagua uwanja wa michezo wa Nanook's wilayani Tunduru. 
 Usafi ukiendelea
 Usafi ukiendelea
 Akizungumza na baadhi ya viongozi 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo.. ameshiriki kufanya usafi kwenye shamba la CCM.. Kijiji cha Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Songea.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.