Habari za Punde

SERIKALI YA TANZANIA BARA KUSHIRIKIANA KATIKA SOKA NA ZANZIBAR

 Na Shamimu Nyaki WHUSM
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Habari,Utalii Utamaduni na Michezo ya Zanzibar zimekubaliana kushirikiana katika Michezo ikiwa ni mikakati ya kuleta mafanikio ya soka ndani na nje ya nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa lengo la kukutana na Waziri mwenye Dhamana ya Michezo visiwani Zanzibar ni kutimiza lengo la muda mrefu la kukutana na kupanga mikakati mbalimbali ya kuinua soka la nchi hizo.
“Tumekutana kuweka mikakati imara ya kutimiza lengo la muda mrefu la kutafuta na njia mbalimbali zitakazosaidia soka letu kukua na kuimarika ndani na nje ya ya nchi zetu”,Alisema Dkt.Mwakyembe.
Aidha ameipongeza Zanzibar kwa kufanikiwa kuwa mwanachama halali wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika(CAF) na ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika maendeleo ya soka ya nchi hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Habari  Utalii Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Mhe.Rashidi Waziri  amesema kuwa Wizara yake ina jukumu kubwa kuendeleza Soka la Zanzibar hasa katika kipindi hiki amabacho imepata nafasi katika Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika.
Mhe. Waziri Rashidi ameongeza kuwa ushirikiano wa Kisoka baina ya Wizara hizo utaleta hamasa kwa wawekezaji wa soka kupata uwanja mpana wa uwekezaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
“Tanzania ina matarajio makubwa sana kwakuwa kwa kipindi kirefu tumekuwa wasindikizaji hivyo ushirikiano ni njia pekee ya kuweza kutatua changamoto ya kuingia katika soka la FIFA”

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.