Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA UJENZI AWAMU YA KWANZA RELI YA TRENI YA UMEME YA DAR- MORO

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akiweka Jiwe la Msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Treni ya Umeme awamu ya kwanza kutoka jijini Dar es Salaam, mpaka Morogoro,wakati wa hafla ya uzindzu na uwekaji Jiwe hilo iliyofanyika Pugu jijini leo.
Rais Dkt. John Magufuli, akikata utepe kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Treni ya Umeme awamu ya kwanza kutoka jijini Dar es Salaam, mpaka Morogoro,wakati wa hafla ya uzindzu na uwekaji Jiwe la msingi iliyofanyika Pugu jijini leo. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Dkt. John Magufuli, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi na uwekaji Jiwe la msingi Ujenzi wa awamu ya kwanza wa Reli ya Treni ya Umeme kutoka jijini Dar es Salaam,kwenda Morogoro, iliyofanyika Pugu jijini.
 Rais Dkt. John Magufuli, akichanganya mchanga kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Reli ya Treni ya Umeme kutoka jijini Dar es Salaam, kwenda Morogoro iliyofanyika Pugu jijini, leo.
 Rais Dkt. John Magufuli, akiinama kugusa chuma cha Reli kujua ubora wake baada ya uzinduzi huo. Kulia ni Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Hamphrey Polepole,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, wakiwa wamechuchumaa, kwenye mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na  Hawa Ghasia (Mb). 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Hamphrey Polepole, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema,wakati wa hafla ya uzinduzi na uwekaji Jiwe la msingi Ujenzi wa awamu ya kwanza wa Reli ya Treni ya Umeme kutoka jijini Dar es Salaam,kwenda Morogoro, iliyofanyika Pugu jijini, leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katika katika ya mfano wa Reli hiyo itakayojengwa. 
 Rais Dkt. John Magufuli, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa, wakati wa hafla ya uzinduzi na uwekaji Jiwe la Msingi kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Treni ya Umeme awamu ya kwanza kuanzia jijini Dar es Salaam, kwenda Morogorogo, iliyofanyika Pugu leo.

 Picha ya pamoja.....
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakary Zubeiry mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
  Rais Magufuli akipunga mkono kuaga wananchi wakati akiondoka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza msanii Mrisho Mpoto mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Pugu jijini Dar es Salaam. 
 Msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto, akitumbuiza kwa kughani mashahiri yake kuhusu uzinduzi huo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt. Magufuli.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.