Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA MABWENI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, KAMPASI YA MLIMANI, AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA 644 ZA MAGOMENI KOTA, DAR.

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli, akingozana na baadhi ya viongozi, akitembelea kukagua ujenzi wa majengo ya Nyumba 644 za Magomeni Kota, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa nyumba hizo, iliyofanyika Magomeni jijini Dar es Salaam. 
RAIS Dkt. John Magufuli, Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, (wa pili kushoto) Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto) na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole (kulia) kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi Mabweni ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika katika viwanja vya majengo hayo, jijini Dar es Salaam.
********************************************
Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutowachagulia vyuo wanafunzi wa elimu ya juu na kuwaacha wanafunzi hao kuchagua vyuo wanavyovitaka wenyewe.
Agizo hilo limetolewa leo, Jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alipokuwa akizindua Mabweni mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa Chuoni hapo Juni, mwaka jana.
“Ninaamini kama wanafunzi wangepewa nafasi ya kuchagua vyuo wanavyovipenda wenyewe, vyuo vya Serikali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Mzumbe vingekuwa na wanafunzi wengi sana,” alisema Dkt. Magufuli.
Aliendelea kwa kusema kuwa TCU imekuwa ikiwachagulia wanafunzi vyuo visivyo na sifa na makazi ya wanafunzi hivyo kusababisha wanafunzi hao kusoma katika mazingira magumu na wanapomaliza masomo yao hukosa ajira kutokana na vyuo hivyo kutokuwa na sifa.
Aidha, Rais Magufuli ameuagiza uongozi wa UDSM kutoza wanafunzi gharama ya shilingi mia tano(500) kama malipo ya makazi ya mabweni hayo kwa siku badala ya shilingi mia nane(800) inayotozwa kwa mabweni mengine yaliyopo chuoni hapo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuwekeza katika elimu hivyo itahakikisha wanafunzi nchini wananufaika kwa kupata elimu bora kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.
“watanzania walinichagua ili kutatua changamoto zinazowakabili na hivi ndivyo ninavyofanya kutatua changamoto hizo” alisema Rais Magufuli.
Naye, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amempongeza Rais Magufuli kwa kutoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo ambao kwa kiasi kikubwa yatatatua changamoto ya makazi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa chuo hicho.
Prof. Ndalichako amesema kuwa mabweni hayo yamejengwa kwa kipindi cha miezi 8 ambayo yatachukua wanafunzi 3840.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala ametoa rai kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanaimarisha usalama katika maeneo ya mabweni hayo na kulinda miundo mbinu yote iliyoweka.
“Ni lazima mzingatie matumizi sahihi ya kila kifaa kilichofungwa katika majengo haya, majengo haya ni mapya na yamejengwa kwa gharama kubwa kwa lengo la kutusaidia kuondokana na changamato iliyotukabili kwa muda mrefu,” alisema Prof. Mukangala.
Dkt. John Pombe Magufuli, Mwajuma Hamis, Mkazi wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota, na baadhi ya viongozi wakikata utepe  kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba 644 za Magomeni Kota wakati wa hafla iliyofanyika, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Dkt. John Pombe Magufuli, Mwajuma Hamis, Mkazi wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota, wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba 644 za Magomeni Kota wakati wa hafla iliyofanyika, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie, waliohudhuria hafla hizo wakimsikiliza Rais Dkt. Magufuli.
Baadhi ya Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM, na wanachi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa Mabweni ya wanafunzi wakimsikiliza Rais wakati akihutubia. 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Mabweni ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani, wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja
Baadhi ya waliokuwa wakzi wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota
Picha ya pamoja baada ya kukata utepe
Rais Magufuli akiagana na baadhi ya wasanii wa Bongo Movie, Dkt. Chein na wenzake.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akifurahia jambo na Msanii wa Maigizo 'Bongo Movie', Jacob Steven (JB), baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba 644 za Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Magufuli akiagana na Bi. Mwajuma Hamis
Rais akipunga mkono kuwaaga wananchi
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akipiga Tumba za bendi ya Msondo Ngoma waliokuwa wakitoa burudani katika hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba 644 za Magomeni Kota jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.