Habari za Punde

SERENGETI BOYS YAANZA VYEMA MECHI ZAKE ZA KIRAFIKI IKIWA KAMBINI MOROCO

TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imeanza vyema mechi zake zakirafiki kwa kuibanjua Gabon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa mjini Rabat, Morocco.
Wafungaji wa mabao hayo, ni Kelvin Nashon Naftali dakika ya 18 na Ibrahim Abdallah Ally dakika ya 75.
Serengeti Boys imeweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28, mwaka huu nchini Gabon.
Serengeti Boys itakuwa kambini mjini Rabat hadi Mei 1, mwaka huu itakapowenda Younde, Cameroon kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Mei 3 na 6, mwaka huu.
Mei 7 timu hiyo itakwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola, wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.