Habari za Punde

SERENGETI BOYS YACHOMOA JIOOOONI KWA GHANA U17 2-2

 Beki wa timu ya Vijana wa U 17 ya Tanzania Serengeti Boys, Nickson Kibabage (kulia) akiruka kupiga shuti langoni mwa Ghana, huku akizongwa na beki wa Ghana U17, Antwi Nana Kamwe, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa wa timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jioni ya leo. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2. 
 Winga wa Serengeti Boys Yohana Mkomola (kushoto) akimtoka beki wa Ghana U17,  Yusif Abdulrazak, wakati wa mchezo huo. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Beki wa Ghana U17,Sulley Ibrahim (kushoto) akichuana kuwania mpira na Assad Juma, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa wa timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Beki wa Serengeti Boys, Israel Mwenda (kushoto) akipiga krosi mbele ya mchezaji wa Ghana, Toku Emmanuel, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa wa timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha Serengeti Boys
 Kikosi cha Ghana U17
 Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza kuwashangilia Serengeti Boys
 Waziri Mwakyembe, akisalimiana na wachezaji wa serengeti Boys kabla ya mchezo huo kuanza.
 Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe akimkabidhi bendera ya Taifa, Nahodha wa timu ya Vijana wa U 17 ya Tanzania Serengeti Boys, Ally Msengi,wakati wa  wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa wa timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini wiki hii. 
Waziri Mwakyembe akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.