Habari za Punde

SPIKA NDUGAI AKAGUA TIMU NETIBOLI YA BUNGE.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia) wakati akikagua kikosi cha timu ya netball ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya timu ya netball ya Bunge la Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Mchezaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jezi ya rangi ya bluu bahari, akifunga goli dhidi ya timu ya Bunge la Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo wa netball uliochezwa leo katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.