Habari za Punde

TALIS, DAR SWIM CLUB ZANG'ARA KLABU BINGWA MCHEZO WA KUOGELEA

Mwakilishi wa benki ya CRDB akimpongeza muogeleaji nyota wa Tanzania anayesoma Uingereza kwenye shule ya St Felix baada ya kushinda medali ya dhahabu.
Romeo mihaly wa Champion Rise akipozi na Tan Liu wa Taliss na Saffiro Kweka wa DSC baada ya kushinda medali. 
Muogeleaji wa Tanzania anayesoma shule ya St Felix,Collins Saliboko ' akipambana' katika mashindano ya Taifa.
******************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Klabu kongwe ya mchezo wa kuogelea Tanzania, Taliss imeshinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya kuogelea ya klabu bingwa yaliyofanyika kwa siku mbili kwenye bwawa la kuogelea la Hopac, Kunduchi jijini.
Klabu hiyo imejikusanyia pointi 3,587  katika mashindano magumu na ya kusisimua yaliyoandliwa na Chama Cha Kuogelea nchini (TSA) na kudhaminiwa na Davis & Shirtliff, CRDB Bank, Mediterraneo Hotel & Restaurant, Coca Cola, Aggrey & Clifford na  The Terrace.
Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka amesema kuwa Taliss iliweza kujikusanyia pointi 1,681 kwa upande wa waogeleaji wa kike wakati kwa upande wa waogeleaji wa kiume, klabu hiyo ilipata pointi 1,886.
Namkoveka alisema kuwa nafasi ya pili ilichukuliwa na klabu nyota  ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC) kwa kupata pointi  2,587 . klabu hiyo ilipata pointi 1,564  kwa upande wa wanawake na pointi 663 kwa upande wa wanaume.
Nyota kadhaa wa mchezo huo nchini chini ya muogeleaji namba moja nchini kwa upande wa wanawake, Sonia Tumiotto na wenzake,  Smriti Gorkarn, Celina Itatiro, Anjan Taylor na Maia Tumiotto  waliweza ‘kufunika’ katika mashindano hayo kwa kuwa na ‘kasi ya ajabu.
Klabu ya Morogoro  maarufu kwa jina la Mis Piranha ilimaliza katika nafasi ya tatu kwa kupata pointi 1,434. MIS ilipata pointi 606 kwa upande wa wanawake na jumla ya pointi 828 kwa upande wa wanaume.
Waogeaji wa klabu ya Mwanza (MSC) walishika nafasi ya nne kwa kupata pointi 1,122 huku klabu ya Zanzibar, Wahoo ikimaliza katika nafasi ya nne kwa kupata pointi 497. Nafasi ya tano ilichukuliwa na klabu ya Bluefins kwa kupata pointi 442 wakati Champion Rise ikiibuka ya sita kwa kupata pointi 221.
Klabu za Moshi iliopata pointi, KMKM, Kennedy House School, Zanzibar Dolphins, , Heaven of Peace academy  na JKT zilimaliza katika nfasi ya saba mpaka ya 13.
Namkoveka alisema kuwa mashindano hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na maandalizi mazuri na sapoti kutoka kwa wadhamini.
 “Tunashukuru kumaliza salama mashindano haya, kwa kweli yalikuwa magumu na kwa mara ya kwanza, jumla ya waogeleaji 172 walishiriki, hii ni ishara kuwa mchezo wetu unakuwa na tunatarajia kupata mafanikio zaidi katika timu zetu za taifa,” alisema  Namkoveka.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.