Habari za Punde

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA SOKA DUNIANI

Hivi karibuni, Tanzania ilifanya vizunri katika mechi za Kimataifa za kirafiki za kalenda ya FIFA, baada ya kuwashinda Botswana kwamabao 2-0 na Burundi kwamabao 2-1 katika michezo iliychezwa Machi, mwaka huu.
Katika viwango hivyo vipya vya mwezi April, Brazil imeishusha Argentina kileleni na kukamata usukani rasmi wa dunia, huku Argentina ikishuka hadi nafasi ya pili na Ujerumani ikibaki katika nafasi yake ya 3.
Katika ‘Top Ten’, mataifa yanayofuata ni Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswisi na Hispania inakamata nafasi ya 10
Barani Afrika Misri inaongoza ikiwa nafasi ya 19 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 30, Cameroon nafasi ya 33, Burkina Faso nafasi ya 35, Nigeria nafasi ya 40 na Congo DR nafasi ya 41 ikiwa mbele ya Tunisia kwa nafasi moja
Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda bado inaongoza ikiwa imepanda kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 72, ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 78, Rwanda nafasi ya 117, Ethiopia nafasi ya 124, Tanzania nafasi ya 135 na Burundi imeshuka kwa nafasi mbili hafasi ya 141.
Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 194 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.