Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo
Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusinano na Mipango wa TPDC, Nathan Mnyawami.
Baadhi ya waaandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) uliofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
*********************************************************
Na:
Frank Shija – MAELEZO.
TPDC
kwa kushirikiana na Sekta binafsi wanatarjia kutekeleza miradi mbalimbali ya
usambazaji wa gesi asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara
na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.
Hayo
yamebainishwa na Kiamu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba
wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es
Salaam.
Mhandisi
Musomba amesema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi
wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam,
ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017 TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo
yalikidhi vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.
“Napenda
kuutaarifu umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji
wa gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani
Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema Mhandisi
Muyomba.
Aliongeza
kuwa lengo la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za
kifedha, mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji
wa kanda za usambazaji.
Aidha
alisema kuwa ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na
kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu
itakayowezesha usambazaji wa gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu
mapitio ya upembuzi yakinifu utakapomalizika.
Mtandao
huo unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa
kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na
vituo vya kujazia gesi hiyo.
Katika
hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa hadi sasa TPDC
imefanikiwa kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja cha
kutengeneza Vigae cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku
likiendelea na majadiliano na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya kuunganishwa
na mtandao huo.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika rasmi
la taifa linalojiendesha kibiashara, ambapo sheria hii inaipa mamlaka TPDC
kuruhusu makampuni mbalimbali kuendesha shughuli za sekta, zitakazokuwa
zainadhibitiwa kwa utaratibu maalum chini ya usimamizi wa Mdhibiti anayetoa
leseni.
No comments:
Post a Comment