Habari za Punde

TRL WAZINDUA SAFARI YA TRENI YA MIZIGO KWENDA MKOANI DODOMA, BAADA YA ILE YA KWANZA KWENDA BURUNDI

Mwenyekiti wa Bodi wa TRL, John Kondoro, akipeperusha bendera kama ishara ya kuzindua na kuruhusu kuanza kwa safari ya Treni ya Mizigo kuelekea mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Treni hiyo ni ya pili kuanza safari baada ya Treni ya kwanza kuzinduliwa na kuanza safari yake kwenda nchini Burundi, mwezi uliopita.
  Mkurugenzi Mwakilishi Mkaazi kutoka WPF, Michael Dunford, akimkabidhi 'Line Clear' dereva wa Treni ya mizigo iliyoanza safari zake kutoka jijini Dar es Salaam, kuelekea mkoani Dodoma, ikiwa kama ishara ya kuiruhusu Treni hiyo kuanza safari hizo, wakati wa uzinduzi uliofanyika leo. Treni hiyo ni ya pili kuanza safari baada ya Treni ya kwanza kuzinduliwa na kuanza safari yake kwenda nchini Burundi, mwezi uliopita.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TRL, Masanja Kadogosa, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mwakilishi Mkaazi wa WPF, Michael Dunford, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya TRL, John Kondoro (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TRL, Masanja Kadogosa,wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TRL, Masanja Kadogosa, akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.