Habari za Punde

UMOJA WA ULAYA WAIPATIA SERIKALI YA TANZANIA MSAADA WA BILIONI 490

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James Magosha, (kushoto) akibadilishana mkataba wa msaada wa sh. Bilioni  490 na Mkuu wa Msafara wa Ujumbe wa Jumuiya ya Ulaya kwa Tanzania na Nchi za Afrika Mashariki,  Roeland Van de Geer, wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba huo iliyofanyika kwenye Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, jana. Mkatabha huo ni kwa ajili ya kusaidi Bajeti ya Serikali ya mwaka huu. 
 Wakitiliana saini
 Mkutano ukiendelea, Katibu mkuu akisoma hotuba yake.
Katibu Mkuu akizungumza na kujibu maswali ya waandishi. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
*****************************************
Na Daudi Manongi - MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini msaada wa shilingi Bilioni 490 usiokuwa na masharti yeyote kutoka Umoja wa Ulaya ikiwa ni msaada wa kibajeti kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka wa bajeti wa 2017/18. 
Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema Umoja wa Ulaya umetoa msaada huo kutokana na kuvutiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
“Nadhani mmeshuhudia utiaji saini huu ulioisha hivi punde na Umoja wa Ulaya wametuhakikishia kuendelea kutusaidia katika masuala ya misaada ya kibajeti pamoja na kuwa bega kwa bega na Serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo”,Aliongeza Katibu Mkuu huyo.
Pamoja na hayo mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa wa Bajeti ya mwaka 2017/18 pia utapewa msaada na umoja huo kwani wameuona mpango huo una tija na kuweka mkazo  katika viwanda na kilimo.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Roeland Van de Geer amesema kuwa wameliangalia zaidi suala la utawala kama eneo kuu katika mpango wa ushirikiano na Tanzania na vilevile wanatazamia maendeleo zaidi katika maeneo ya kilimo,ujenzi wa barabara za vijijini na nishati.
“Mkataba ambao tumeusaini utaiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango katika ukusanyaji wa mapato,zitaboresha uwajibikaji na utumiaji mzuri wa mali za Serikali, na Umoja wa Ulaya unasapoti azma ya viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano,”Aliongeza Roeland Van de Geer.
Amesema kuwa ushirikiano uliopo katika ya Tanzia na Umoja wa Ulaya ni mpana sana na utaendelea kuimarika zaidi katika kipindi hiki ambacho mageuzi ya sera yanahitajika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.