Habari za Punde

VIDEO: MBUNGE WA BUSEGA RAPHAEL CHEGENI AFANIKISHA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI YA NGASAMO
Mbunge wa Jimbo la Busega, Mkoani Simiyu, Dk Raphael Chegeni ambaye kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wa ndani na nje ya nchi amefanikiwa kujenga bweni moja la wasichana katika Sekondari ya Ngasamo ikiwa ni jitihada za kuwanusuru watoto wa kike na ukatishaji masomo unaotokana na mimba pamoja na vishawishi bvingine mbalimbali.


Vitanda katika moja ya vyumba vya bweni hilo. 


MBUNGE wa Busega Dr. Raphael Chegeni amefanikisha ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Ngasamo. 
Bweni hilo lenye uwezo wa kuhudumu wanafunzi wa kike 48 litasaidia wasichana kupata muda wa kujisomea na kujiepusha na adha ya kutembea mwendo mrefu wa kuja na kurudi shuleni. 
Kitendo hicho imekuwa kikwazo kwa baadhi kuangukia mtego wa kukatisha masomo katokana na bodaboda Au lift kuwasababishia mimba na hivyo kukatisha masomo yao. 
Mbunge huyo ameweka mpango kujenga mabweni kwa shule zilizo katika mazingira hatarishi zikiwemo Malili, Mkula, Kabita na Sogesca. 
Aidha amewashukru wadau wakiwemo ubalozi wa Ireland, Canada, Tanapa na Serikali kwa kuchangia jitihada hiz0.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.