Habari za Punde

WANACHAMA YANGA WAZINDULIWA AKAUNTI YA KUCHANGIA TIMU, WACHEZAJI WAPONGEZWA KUTINGA NUSU FAINALI ASFC

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam,leo.
***********************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KLABU ya Yanga imewapongeza wachezaji wa timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho 'ASFC'  baada ya kuondisha mashindanoni Tanzania Prisons mabao 3-0 mchezo uliopigwa mwishoni jumamosi wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa. 
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Bonifac Mkwasa,  alizungumza hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Akaunti mpya ya Wanachama wa Yanga watakaoweza kuichangia timu uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkwasa alisema kuwa wanaheshimu uwezo wa Mbao ambapo, wao pia wanajipanga vyema na kujiandaa kupata ushindi katika uwanja wa Kirumba.
Akizungumzia Akaunti hiyo mpya Mkwasa, alisema kuwa Klabu imeamua kuchukua hatua hiyo ya kuzindua Akaunti ya 'mashabiki Changia timu' ili kuweza kuongeza mapato kwa Klabu kupitia mashabiki wao, baada ya timu hiyo kuyumba kiuchumi.
Hatua iliyochukuliwa ni kufungua akaunti maalumu ambayo itawapa fursa wapenzi , wanachama, mashabiki na wadau wa timu hiyo kuichangia fedha klabu yao ili kuipa nguvu na hamasa ili kuendelea kufanya vizuri katika michezo ya Ligi baada ya kutofanya vizuri katika mechi zake za kimataifa.
"Niwaombe tu mashabiki na wanachama wetu watuunge mkono katika kipindi hiki kigumu kwa kuichangia timu yao na sisi kama uongozi tumeona ni jambo lenye tija . Hii haina tafsiri ya kwamba klabu haina fedha na imekwama kabisa kujiendesha bali tumelipitisha ili kukidhi matakwa ya wengi," alisema Mkwasa. 
Mkwasa alisema kuwa anafahamu wote wanaokuja uwanjani au kulipia kadi kama sehemu ya kuongeza mapato ya klabu lakini kwa mfumo huu ambao tunaenda kuuzindua utatoa fursa kwa kila mdau popote alipo kuichangia klabu kama sehemu ya kujivunia timu hii na kusimama kama nguzo muhimu ya maendeleo ya klabu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.