Habari za Punde

WANAHABARI WAELIMISHWA KUHUSU TOFAUTI YA KODI YA PANGO LA ARDHI NA KODI YA MAJENGO


   Kaimu Kamishna wa Ardhi, Willson Paul Luge, akizungumza wakati akifungua rasmi Semina kwa Waandihi wa Habari kuhusu tofauti ya Kodi ya Pango la Ardhi na Kodi ya Majengo, iliyofanyika leo Ofisi za Wizara hiyo Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Ofisa Kodi Mkuu kutoka TRA Makao Makuu, Sydney Mkaba (kulia) ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Mboza Lwandiko. 
 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Mboza Lwandiko, akizungumza wakati wa semina hiyo.
  Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami, akitoa mada kwa washiriki wakati wa Semina kwa Waandihi wa Habari kuhusu tofauti ya Kodi ya Pango la Ardhi na Kodi ya Majengo, iliyofanyika Ofisi za Wizara hiyo Dar es Salaam, leo. Semina hiyo ilifunguliwa na Kaimu Kamishna wa Ardhi, Willson Paul. 
*****************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WANANCHI wametakiwa kuelewa tofauti ya Kodi ya Majengo na kodi ya pango la ardhi ili kuweza kulipia kodi husika kwa wakati bila kujali kuwa ardhi husika imeendelezwa ama haijaendelezwa.
Hayo yamesemwa na Kaimu Kamishna wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Willson Paul, wakati akifungua Semina ya siku moja kwa Waandishi wa Habari, kuhusu tofauti ya Kodi hizo, iliyofanyika Ofisi za Wizara hiyo Dar es Salaam, jana.
Aidha Willson alisema kuwa wananchi walio wengi hawatambui tofauti hizo ambazo kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999, ambayo imekabidhi mamlaka kwa Wizara ya Ardhi iweze kukusanya kodi kwa yeyoye anayemiliki ardhi, ambapo mmiliki aliyepewa umiliki na Serikali ni lazima eneo lake lipimwe na kupata Documenti za Serikali na kupata Hati ili kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.
''Dhana hii inatokana na Sheria ya Ardhi No. 4  ya mwaka 1999 katika fungu la 3 kifungu kidogo cha 1 (a) kinachosema:
 ‘Itambulike kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya Umma iliyowekwa chini ya Mheshimiwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi’,
Hivyo sera ya ardhi ya mwaka 1995 imempa mamlaka Mh. Rais kumiliki ardhi kwa niaba ya wananchi, na wananchi wamepewa haki ya kutumia ardhi kwa masharti ya sheria''. alisema Willson
Alisema kuwa mfumo huu wa umiliki wa ardhi unatambulika kama 'lease hold na sio free hold'. Kwa mantiki hiyo aina hii ya umiliki yani 'lease hold' ni upangaji katika ardhi ambao mpangaji anawajibika kufata masharti ya upangishaji na mojawapo ya masharti hayo ni pamoja na kulipa pango la kipande cha ardhi. 
Kodi ya Pango la Ardhi huanza kulipwa kila mwaka ambayo huanza rasmi Julai Mosi, huku Kodi ya Majengo hutozwa kwa jengo ambalo limejengwa kwa vifaa vya kudumu, ambalo linatumika au kukaliwa na liwe katika mamlaka ya majiji, Miji midogo na Manispaa.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami, wakati akitoa madaka katika semina hiyo alisema kuwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  ilikasimiwa zoezi la kukusanya kodi na tozo mbalimbali  zinazotokana na sekta ya ardhi, kuanzia mwaka  wa fedha  1996/1997, ambapo awali kodi hizi zilikuwa zikikusanywa na Serikali Kuu kabla ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 
Akielezea kuhusu Changamoto alisema kuwa ni baadhi ya wamiliki kuchanganya kati ya kodi ya pango la ardhi  na kodi ya Majengo, ambapo Wizara hutumia nguvu nyingi kutoa elimu hiyo kwa wananchi na walipa kodi kwa ujumla kwa kutumia semina.
Pia alizitaja baadhi ya Changamoto hizo kuwa ni kuchelewa kuchukua hatua za kisheria na hivyo huchelewesha zoezi zima, Tatizo la kumbukumbu kuwa baadhi ya wadaiwa wanalipa lakini hawafiki kuhuhisha kumbukumbu na hivyo wakati wa kutekeleza zoezi hilo wanajitokeza hatua za mwisho kabisa jambo ambalo huwafanya wahusika kufanya kazi mara mbili na kupoteza muda na lasilimali fedha nyingi bila ya manufaaa.
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo. wakimsikiliza mgeni rasmi.
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo. wakimsikiliza mgeni rasmi.
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo. wakiwa bize kusoma makablasha husika katika semiana hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami, akifafanua jambo kwa washiriki.
 Ofisa Msaidizi wa Huduma na elimu kwa Mlipa Kodi, Maya Magimba, akitoa mada kwa washiriki kuhusu ulipaji kodi.
 Meneja wa Kitengo cha Elimu ya Mlipa Kodi kutoka TRA, Gabriel Mwayosi (kushoto) akifafanua jambo kwa washiriki, wakati wa Semina hiyo.
Ofisa Kodi Mkuu kutoka TRA, Sydney Mkamba, akifafanua jambo kwa washiriki, wakati wa Semina hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.