Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA KUTETA NA UONGOZI WA SIMBA MJINI DODOMA

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo , Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Klabu ya Simba, ukiongozwa na Rais wake, Evans Aveva Mjini Dodoma, jana. 
*******************************************
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe jana alikutana na uongozi wa klabu ya Simba ukiongozwa na Rais wake, Evans Aveva kwenye Ofisi zake Mjini Dodoma.
Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Waziri Mwakyembe wa kukutana naye na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa Miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maedneleo ya uendeshaji wa timu.
Aidha, Mwakyembe  amepokea maoni ya Uongozi wa Simba na kushauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu nchini.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa  na Katibu Mkuu Wizara husika Prof.  Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja, na Msajili wa Vilabu na Vyama nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja  na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva Mjini Dodoma.  Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM Dodoma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.