Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA NGOMA NA MUZIKI ASILI TANZANIA

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) wakati alipokutana nao Ofisini kwake Mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya Sanaa za Ngoma na Muziki Asili Tanzania Leo April 21, 2017.
Mwenyekiti wa Chama cha Ngomana Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Wanne Salim Kutoka Kikundi cha  Wanne Star  akieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii wa Ngoma na Muziki Asili kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21, 2017.
Katibu wa Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Richard Muro  akifafanua jambo  kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21,2017.
Mmoja wa wasanii kutoka Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Zuhura Khatib akimueleza jambo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21, 2017. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.