Habari za Punde

WLAC KUENDESHA MABONANZA ILI KUWAFIKISHIA VIJANA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA

'' Jaribu hii uchekeshe walionuna''
 Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC) Abia Richard, akizungumza wakati wa Tamasha la Vijana la kupinga Ukatili wa Kijinsia lililofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. , Katikati ni mgeni rasmi, Ofisa Maendeleo wa Kata ya Tandika, Janeth Mwakibete. Picha zote na Nasma Mafoto
Mgeni rasmi, Ofisa Maendeleo wa Kata ya Tandika, Janeth Mwakibete, akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa Bonanza la Michezo kwa Vijana la kutoa elimu juu ya kuondokana na aina zote za Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake, lililofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.
**********************************
 Na Ripota wetu Nasma Mafoto, Dar
WANAMICHEZO wametakiwa kutumia nafasi zao katika kuelimisha jamii kwa suala zima la vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.
Hayo yalisemwa na Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC) Abia Richard wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Michezo kwa vijana lililofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Wachezaji wa Simba Queens na Mburahati Queens, akichuana kuwania mpira wakati wa Bonanza hilo. Katika mchezo huo Mburahati Queens, waliibuka washindi kwa mikwaju ya penati 4-3. Picha na Nasma Mafoto
 Wafanyakazi wa WLAC wakiwaandikisha wananchi kujitolea kushiriki kampeni ya kupinga ukatili wa Kijinsia.
********************************
Aidha Abia, alisema kuwa katika kipindi hiki cha Utandawazi, wanamichezo wana nafasi kubwa katika kupiga kelele za kupinga unyanyasaji na kukemea vitendo vya ukatili katika mazingira wanayoishi , jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
''Tumeamua kuwatumia zaidi wanamichezo na michezo kwa ajili ya kutoa elimu ya kupinga ukatili, tunaamini kuwa katika kufanya mabonanza kama haya tuliyoanzisha yatasaidia zaidi kuwakusanya watu wengi kwa pamoja na kupata elimu ya jinsi ya kukabiliana na jinsi ya kupinga ukatili wa Kijinsia na hasa kwa mtoto wa kike,
 Elimu ikitolewa kwa vijana
***************************************
Licha ya kutumia wanamichezo, lakini pia Kituo chetu kimepanga kuwashirikisha madereva wa Bodaboda katika kampeni hii ya kupinga ukatili ili kuelimisha jamii,kutokana na wao kufanya kazi kwa ukaribu na jamii, na pia wanaweza kwani wao wakipata elimu hii kwa upeo mkubwa na wao wataweza kuwaelimisha wati wanaowazunguka katika mazingira ya kazi zao''. alisema Abia
Aidha alisema kuwa mkakati uliopo kwa sasa ni kuhakikisha Wananchi wanapata elimu ya kutoka kuhusu unyanyasaji na ukatili na umuhimu wa kuheshimiana na kulinda utu wa mtu bila kumfanyia vitendo vya ukatili.
 Wasanii wa Kikundi cha Talent Search wakitoa burudani katika Bonanza hilo.., kijana akionyesha umahiri wake wa kugandisha Chupa kwenye ubapa wa Kisu.
 Mchezaji wa soka akisebeneka na msanii wa kundi la Talent Search...Picha Zote na Nasma Mafoto
 Viongozi wakikagua timu kabla kuanza kwa mchezo wa soka kwa upande wa wanaume
 Kikosi cha Simba Queens
Kikosi cha Mburahati Queens

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.