Habari za Punde

YANGA YAUNGANA NA SIMBA HATUA YA NUSU FAINALI ASFCMshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akiwa hewani baada ya kuchezewa faulo na kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo (kushoto).
******************************
YANGA SC leo imeungana na timu tatu za Simba SC, Azam Fcna Mbao Fc, kutinga hatua ya Nusu fainali Kombe la Shirikisho, ' Azam Sports Federation Cup' (ASFC) baada ya kuibuna na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa mwisho wa Robo fainali uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Droo ya Hatua hiyo ya Nusu Fainali inatarajiwa kuchezeshwa kesho Saa 11:00 jioni katika studio za Azam TV, zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam.

Winga wa Yanga Simon Msuva, akiruka kupiga mpira wa kichwa katikati ya mabeki wa Tanzania Prisons, wakati wa mchezo huo.

***********************************
Mabao ya yanga yalifungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 15 akimalizia kazi nzuri ya Geofrey Mwashiuya, bao la pili lilifungwa na Obrey Chirwa katika dakika ya 40 akiitendea haki korosi ya Haji Mwinyi, na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, akiruka kupangua mpira wa hatari langoni kwake.
****************************************
Kipindi cha pili, Yanga walikianza kwa mabadiliko, kipa wa tatu Benno Kakolanya aliyeanzishwa leo akitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kipa wa kwanza, Deo Munishi ‘Dida’. 
Na mwanzoni tu mwa kipindi hicho, winga Simon Happygod Msuva akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya 46 kwa shuti kali.
Dida akaokoa mkwaju wa penalti wa Victor Hangai dakika ya 55 uliotolewa baada ya Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumchezea rafu Meshack Suleiman.

Emmanuel Martine wa yanga (kushoto) akiwania mpira na beki wa Tanzania Prisons.

Obrey Chirwa wa Yanga leo alikuwa katika ulinzi mkali,hapa akidhibitiwa na mabeki wawili wa Tanzania Prisons.

Kama vita vile, Chirwa akiminywa na mabeki hao....''mpira uende wewe ubaki''

Chirwa Chiniiiiiiii, kipa kadaka...........

Amis Tambwe akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Prisons.

Msuva akichanja mbuga.....

Mashabiki wa Yabga wakishangilia.....

Winga wa Yanga Simon Msuva, akijikunja kupiga krosi langoni kwa wapinzani Tanzania Prisons, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Kiungo wa Yanga Thaban Kamusoko, akijaribu kuwatoka wachezaji wa Tanzania Prisons. 

Beki wa Tanzania Prisons, Leonsi Mutalemwa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Yanga, Hassan Kessy, wakati wa mchezo wa mwisho wa Robo fainali Kombe la Shirikisho, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Yanga wakishangilia.

Hassan Kessy akijaribu kuwapia mabeki wa Tanzania Prisons.

Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya kufunga bao katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.