Habari za Punde

YANGA YAWAKIMBIZA WAARABU ILA KABAO KAMOJA TU 1- 0

 Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (kulia) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Mc Alger, Awady Said (katikati) na Hachoud Abdullman, wakati wa mchezo wa hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar esSalaam. Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa bao 1-0.
*******************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya hatua ya mtoano ya kombe la Shirikisho Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria, jioni ya leo katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa Kila upande kusaka goli la kuongoza lakini umakini wa safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Mzambia Obrey Chirwa ilishindwa kutumia nafasi walizopata.
Hadi mapumziko matokeo yalikuwa ni 0-0. Kipindi cha pili kilianza kwa MC Alger kulisakama lango la Yanga lakini umakini wa safu ya ulinzi ilikuwa makini na kuondosha hatari langoni mwao.
Kocha George Lwandamina aliamua kufanya mabadiliko ya kwanza na kumtoa Deus Kaseke, nafasi yake ikichukuliwa na Donald Ngoma, na Emmanuel Martine akachukua nafasi ya Haruna Niyonzima, ambapo madiliko hayo yalibadili mchezo na katika dakika ya 61 Thaban Kamosoko, aliiandikia Yanga bao la kuongoza na la ushindi katika mchezo huo.
Yanga walianza kubadilika na kuendelea kulisakama lango la MC Alger lakini Chirwa, alionekana kutokuwa makini zaidi siku yaleo na kutokuwa na bahati kutokana na mashuti yake yote kuwa yakipangiliwa na kipa.
Baada ya matokeo hayo, mechi ya marudiano inatarajiwa kupigwa mnamo April 15 nchini Algeria, ambaoo Yanga inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi au sare ya aina yoyote ili kufuzu kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.
 Chirwa akipambana....
 Chirwa akipiga kichwa na mpira kupanguliwa na kipa
 Hili ndilo bao la Kamusoko
 Beki wa Yanga Hassan Kessy (kushoto) akichuana kurajibu kuwatoka wachezaji wa Mc Alger, Kacem Mehdi (katikati) na Mebarakou Zidane, wakati wa mchezo wa kombe la Shirikisho uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kamusoko akibinjuka kupiga tik tak
 Msuva akichuana kuwania mpira na beki wa Alger
 Donald Ngoma (kushoto) akiwania mpira na beki wa Alger
Heka heka langoni mwa Alger

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.