Habari za Punde

ABDULRAHMAN MUSSA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI APRILI, 2017

Mchezaji wa timu ya Ruvu Shooting FC, Abdulrahman Mussa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Aprili kwa msimu wa 2016/2017.
Abdulrahman aliwashinda wachezaji Jafar Salum wa Mtibwa Sugar FC na Zahoro Pazi wa Mbeya City.
Katika mwezi wa Aprili kulikuwa na raundi tatu na timu ya Ruvu Shooting ilicheza michezo miwili ambayo Abdulrahman alicheza dakika zote 180 na kufunga magoli manne(4) kati ya matano yaliyofungwa na timu yake na hivyo kuifanya timu yake kufikia nafasi ya tisa(9) kutoka nafasi ya kumi(10) katika msimamo wa Ligi ya Vodacom.
Abdulrahman alifunga Hat Trick (magoli matatu) katika mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Majimaji uliofanyika katika uwanja wa mabatini Mlandizi.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Abdulrahman Mussa atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja (1,000,000/) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.