Habari za Punde

CHEKI HAPA PICHA 7 ZA MSUVA ALIPOUMIA AKITAFUTA BAO LA 14 LA KIATU CHA DHAHABU

Kinara wa ufungaji katika msimamo wa mbio za kuwania Kiatu cha dhahabu, Winga wa Yanga ya Dar es Salaa,Simon Msuva, akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia alipogongana na beki wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jioni ya leo,ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Pamoja na kuumia lakini Msuva alifunga bao la kishujaa la kwanza la kuongoza kwa timu yake dhidi ya Mbeya City baada ya kuruka kupiga kichwa na kugona na beki na mpira kujaa wavuni ambapo pamoja na kufunga bao hilo lakini hakuweza kushangilia wala wenzake kwani alianguka chini na kuondolewana na Machela na kwenda kugangwa na kushonwa nyuzi Nne katika paji lake la uso alipopasuka.
 Wenzake wakimwangalia baada ya kuanguka
 Msuva akipatiwa huduma ya kwanza
Wachezaji wenzake wakimba msaada
Akitolewa nje kwa Machela
Msuva baada ya kushonwa nyuzi Nne

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.