Habari za Punde

HAFLA FUPI YA UWEKAJI SAINI MAKUBALIANO YA VIWANGO VYA HUDUMA BAINA YA MAHAKAMA NA KAMISHENI YA USULUHISHI (CMA)

Kaimu  Mkurugenzi kutoka Kamisheni  ya Usuluhishi na Uamuzis(CMA)Bw. Shanes Nungu (kushoto aliyevaa suti nyeusi) na Afisa Mgavi Mkuu, Bw. Raphael  Towo kutoka CMA  wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Viwango vya Huduma Baina ya Mahakama na Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
 Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (kulia) akisaini Mkataba wa Makubaliano ya Viwango vya Huduma Baina ya Mahakama na Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), huku akishuhudiwa na Mtendaji anayeshughulikia Mahakama Kuu,  Mhe. Samson Mashalla(kushoto). Mkataba huo una lengo la kuhakikisha kwamba Mahakama ya Tanzania na Wadau wa nje  wanaimarisha uhusiano, ikiwemo kutekeleza Mpango Mkakati wa Mahakama wa 2015 hadi 2020. Tukio hilo limefanyika leo tarehe 17.05.2017 katika Ofisi  ya Msajili iliyopo Mahakama Kuu jijini Dares Salaam.
 Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (kulia) akikabidhiana  Mkataba wa Makubaliano ya Viwango vya Huduma Baina ya Mahakama na Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Kaimu  Mkurugenzi kutoka Kamisheni  ya Usuluhishi na Uamuzis(CMA)Bw. Shanes Nungu (kushoto).Mkataba huo una lengo la kuhakikisha kwamba Mahakama ya Tanzania na Wadau wa nje wanaimarisha uhusiano, ikiwemo kutekeleza Mpango Mkakati wa Mahakama wa 2015 hadi 2020.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.