Habari za Punde

HUDUMA YA ZAHATI YA MIMEA SASA YATOLEWA BURE NA KAMPUNI YA YARA TANZANIA LTD

  Afisa Ugani wa Yara Tanzania Andrew Mwangomile akiwaelezea wakulima waliotembelea kwenye duka la pembejeo lengo la Zahanati ya mimea iliyoanzishwa na Yara Tanzania kwa kutumia mfano wa zao la mahindi
 Bwana Shamba Andrew Mwangomile akielezea aina ya virutubisho vinavuohitajika kwenye zao la mahindi na vinavyopatikana kwenye mbolea aina ya YaraMila CEREAL
Mkulima Christopher Nduva (kulia) kwa furaha akipokea maelezo yaliopo kwenye kipeperushi cha mahindi cha Yara Tanzania kutoka kwa Bw. Andrew Mwangomile (kati) baada ya zao lake kugundulika changamoto inayolikabilia. Kulia ni muhusika mkuu wa duka la pembejeo Bw. Antony Kalenga ambapo huduma ya zahanani ya mimea ilitolewa.
*****************************************************
Wakulima wamiminika kwenye duka dogo la pembejeo lilipo Mafinga kwa ajili ya kupeleka mazao yao kwa ajili ya kupata utatuzi. Bwana shamba wa kampuni ya Yara Tanzania Ltd Bw. Andrew Mwangomile (kati) akiwaelezea wakulima walioleta mahindi yao kwa ajili ya kupatia ufumbuzi wa changamoto inazozikumba. Bwana shamba huyo alipohojiwa aliesema, Yara Tanzania tumeandaa huduma maalumu inayoitwa "crop clinic day" (siku ya zahanati ya mimea) huduma hii inafanana na ile binadamu au kiumbe hai yeyote anapohitaji huduma ya kwanza akijisikia kuumwa ili kupata huduma ya kwanza. Kwenye siku hii maalumu wakulima huleta mizizi, majani au zao lenyewe kwa ajali ya bwana shamba kuweza kumsaidia kutatua kwa haraka tatizo linalokabili mmea huo."  
Moja ya kauli mbiu zetu ni mkulima afanikiwe na kuweza kulisha dunia kwa kutoa huduma muhimu zinazoweza kumsaidia mkulima kuzalisha mazao bora na sio bora mazao. Yara Tanzania inahakikisha ili mpango huo utekelezeke ni kusaida wakulima kutatua changamoto mbali mbali ya mazao. Siku ya zahanati kwetu ni muhimu na tunatoa huduma hii Bure kwenye mikoa yote nchini kushikiana na mawakala wadogo na wakubwa. Aliongeza alipohojiwa kwa njia ya simu afisa masoko na mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Linda Byaba

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.