Habari za Punde

JKT RUVU YATANGULIA DARAJA LA KWANZA MAPEMAAAA

MAAFANDE wa timu ya JKT Ruvu leo wamekubli yaishe baada ya kutangulizwa Ligi Daraja la kwanza na Toto Africns kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
JKT Ruvu imebakisha michezo miwili kabla ya kumaliza ligi hiyo, ambapo hata kama itashinda yote itafikisha pointi 30 ambazo haziwezi kuiokoa na janga hilola kushuka daraja.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo msimu huu, timu tatu za mwisho ndiyo zinashuka daraja,  ambapo pia Majimaji ya Songea wamefikisha jumla ya Pointi 29 baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui.
Timu inayoshika nafasi ya nne kutoka chini ni Ndanda FC ya Mtwara yenye pointi 30, wakati African Lyon inashika nafasi ya tano kutoka mkiani ikiwa na pointi 31 sawa na Prisons iliyopo nafasi ya 10 ikiwa na pointi pia 31.
Kwa mazingira hayo baada ya JKT Ruvu kushuka daraja, hivi sasa timu za Majimaji, Toto Africans, Ndanda FC, Lyon na Prisons zitakuwa zikipambana kuepuka janga hilo na yoyote inaweza kuungana na JKT Ruvu.
Katika mchezo wa leo, JKT Ruvu ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya nane  mfungaji akiwa Hassan Dilunga, kabla ya Toto kusawazisha dakika ya 20 mfungaji akiwa Waziri Junior kwa kichwa akimalizia krosi ya Mohammed Soud.
Dakika ya 35 Waziri Junior tena aliongeza bao la pili baada ya kutumia vizuri pasi ya Mohammed Soud.
Katika michezo mingine jana, Mwadui ilikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Majimaji ya Songea, huku Ruvu Shooting na Kagera Sugar zikitoka sare ya bao 1-1.

MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA LEO:
Maji maji Fc 3 - Mwadui Fc 0
Azam Fc 3 - Mbao Fc 1
Toto African 2 - JKT Ruvu 1
Ruvu Shooting 1 - Kagera Sugar 1
Yanga 2 - Tanzania Prisons 0

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.