Habari za Punde

MALINZI AOMBOLEZA WANAFUNZI, WALIMU ARUSHA

Shirikisho la 
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa rambirambi ya Sh 500,000 kwa walengwa
walipoteza watoto katika ajali ya gari iliyoua zaidi ya watu 36, wakiwamo 
wanafunzi 33.
Wanafunzi hao 33 
wa darasa la saba, walimu wawili na pamoja na dereva wa gari la shule ya msingi 
iitwayo Lucky Vicent ya Arusha, walifariki dunia jana Mei 6, mwaka huu.
Kwa mujibu wa
taarifa za kipolisi, vifo hivyo vilivyotokea saa 3 asubuhi baada ya gari 
walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu 
mkoani Arusha.
Wanafunzi na 
walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya Tumaini kwa ajili ya 
kufanya mtihani wa ujirani mwema ambako kabla ya kufika basi walilopanda 
liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na 
majeruhi watatu.
Rambirambi hiyo 
ya TFF inakwenda sambamba na salamu za rambirambi zilizotolewa na Rais wa Shirikisho 
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi aliyeungana na viongozi mbalimbali 
akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika kuomboleza
msiba huo.
Katika salamu 
zake za rambirambi, Rais Malinzi amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko 
makubwa taarifa ya vifo hivyo kwani imezima ndoto za watoto waliokuwa 
wakijiandaa kulitumikia taifa katika tasnia mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira 
wa miguu kama wachezaji, makocha, viongozi hapo baadaye.
“Mtazamo wetu 
kwa sasa ni kuendeleza soka la vijana, tena hasa wale walioko mashuleni, hivyo vijana 
wale ni sehemu ya kutimiza ndoto za TFF katika mpira wa miguu hapo baadaye, 
tunakubali haya yote kwa kuwa ni ya Mwenyezi Mungu ndiye anayejua siri,” 
amesema Rais Malinzi.
Salamu za Rais 
Malinzi zimekwenda kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, 
walimu na dereva waliopoteza maisha, akisema: “Huu ni wakati mgumu kwa Wana – Arusha, 
wazazi na walezi hawana budi kuwa na subira kwa sasa.”
Amesema kwamba 
kwa wanafamilia wote wa mpira wa miguu, “Tuwaombee marehemu wote wapumzishwe
mahali pema. Pia wale waliopata majeruhi tunaomba wapone haraka katika ajali 
hiyo mbaya.

Ee Mwenyezi 
Mungu zipumzishe Roho za Marehemu hao, Mahala pema peponi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.