Habari za Punde

MAPACHA WALIOUNGANA WAHITAJI MUME WA KUZANA NAO WATOTO WATATU

Mapacha walioungana Maria na Consolata wakizungumza kwa njia ya simu na mmoja kati ya wasamaria aliyewachangia kiasi cha pesa kupitia simu yao ya kiganjani.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abadalah (kushoto)  akizungumza na mapacha hao.
Mlezi wa mapacha Maria a Consolata akiwatoa darasani kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah picha zote na matukiodaimaBlog
************************************************
Na Ripota Wetu, Iringa
MAPACHA walioungana Maria na Consolata Mwakikuti (26)wakiwa na kiwili wili kimoja huku kila mmoja akiwa na kichwa chake, mikono yake na miguu miwili waliohitimu kidato cha sita shule ya sekondari Udzungwa wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa, wamesema wanatamani kuwa walimu ili kulipa fadhila kwa jamii kwa kuwafundisha watoto wao.
Mapacha hao walisema kuwa baada ya kuhitimu masomo yao hivi sasa hitaji lao ni kuwa na watoto watatu pekee hivyo pindi watakapomaliza chuo kikuu wakianza kujitegemea watahitaji mwamaume wa kuwaoa ili kuanza safari ya kutafuta familia yao ya watoto watatu . KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Wakizungumza mara baada ya sherehe hiyo fupi ya kuwaaga mapacha hao Maria na Consolata kwa kuhitimu masomo yao, walisema wanampongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kuonyesha kuwajali na kuwa wanataraji kuendelea na masomo ya chuo kikuu na baada ya kumaliza masomo ya chuo kikuu wanategemea kuifanya kazi ya ualimu na baada ya hapo kuendesha maisha yao wenyewe kwa kuolewa na kuwa na watoto watatu pekee .
Mapacha hao walimuomba mkuu wa wilaya ya Kilolo kuwakutanisha na makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ama Rais Dkt John Magufuli ili kufikisha ombi lao la kuomba kusaidia kuifanyia ukarabati shule ya sekondari Udzungwa na kusaidia kutatua kero ya vitabu vya masomo ya sayansi shule za sekondari nchini .
"Mheshimiwa mkuu wa wilaya tunaomba sana viongozi kuendelea kuwa waadilifu kama ilivyo kwa Rais wetu Dkt John Magufuli mzee wa hapa kazi Tu .....tunatambua wewe mkuu wa wilaya ni muadilifu sana na ndio maana uliahidi na umetimiza ahadi yako ya kutusaidia na kuwaandalia wanafunzi wenzentu chakula muda wote wa mitihani,
Ila tunaomba iwapo makamu wa rais atafika Kilolo basi tumsubiri tukutane nae au tufikishie salamu zetu kwa rais na maombi yetu hayo " walisema mapacha hao huku wakishuka chini ya kochi walilokuwa wamekaa na kupiga magoti .
Walisema wanashukuru wadau wote ambao wamepata kuwasaidia toka wakianza elimu ya sekondari wilaya ya Kilolo wakiwemo Hamashauri ya Kilolo ambao walijitolea kujenga nyumba yao maalum pia kituo cha Nyota ya asubuhi na wengine wote kwa misaada mbali mbali waliyoipata wakiwa shuleni hapo.
Kwani walisema wamepata kuishi vizuri pamoja na kuwa wao ni watoto watatu kati ya watoto 5 wa familia ya Mwakikuti ambao kwa sasa walikwisha fariki dunia wote wawili kwa maana ya mama na baba waliokuwa wakifanya kazi ya ubwana shamba na bibi shamba wilaya ya Makete wakitokea mkoa wa Mbeya.
Walisema maendeleo yao mazuri shuleni hapo ni kutokana na faraja kubwa ambayo ilikuwa ikionyeshwa na wasamaria wema mbali mbali na kuwa imani yao kubwa na kupata matokeo mazuri zaidi katika mtihani huo wa kidato cha sita .
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia mbali ya kuwapongeza kwa kutambua michango mbali mbali ya wahisani bado alisema iwapo makamu wa Rais wakati wa ziara yake wilaya ya Kilolo atamuomba mkuu wa mkoa wa Iringa ili kumwomba mkamu wa Rais kupita kuwasalimia mapacha hao .
Alisema kuwa pongezi nyingi walizotoa kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli zitamfikia na kuwa bado serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya watanzania wote na kuwa ili kumuunga mkono Rais ,mkuu huyo wa wilaya alitaka wahitimu wa kidato cha sita shuleni hapo kuhakikisha wanaachana na mpango wa kukimbilia kuolewa na badala yake kuendelea na masomo zaidi .
Mkuu huyo wa wilaya alitaka wahitimu hao kuwa mabalozi wema kwa Taifa kwa kujiepusha na matendo yasiyo faa kama utumiaji wa dawa za kulevya na mengine yanayofanana na hayo yasiyo mema kwa jamii. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.