Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA YANGA vs TANZANIA PRISONS JANA

 Beki wa Tanzania Prisons, Michael Ismail, (kushoto) akiruka kuondoa mpira wakati akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,jana. Katika mchezo huo Yanga walishinda mabao 2-0 yakifungwa na Amis Tambwe na Obrey Chirwa
Beki wa Tanznia Prisons, Benjamin Asukile (kulia) akiondoa mpira wa hatari hukub akizongwa na mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
 Heka heka langoni kwa Prisons
Beki wa Tanzania Prisons, Michael Ismail, akiondosha hatari mbele ya Amis Tambwe. KUSOMA NA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

 Mabeki Hassan Kessy na Benjamin
 Chirwa akiwatoka mabeki
KIKOSI CHA YANGA: Benno Kakolanya, Hassan Kessy/Juma Abdul dk59, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’/Haruna Niyonzima dk65, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa/Matheo Anthony dk81 na Geoffrey Mwashiuya.
 KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS: Aaron Kalambo, Benjamin Asukile, Michael Ismail, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya, Mohammed Samatta/Nchinjay Kazungu dk86, Victor Hangaya/Kassim Hamisi dk63, Lambert Sibiyanka na Meshack Suleiman.
Kipa wa Tz Prisons Aaron Kalambo, akipangua mpira
 
 Mwashiuya alipokuwaakijaribu kumchachafya beki wa Tz Prisons
 Niyonzima akifanya yake
Shabiki wa Yanga akila ubwabwa na kuku jukwaani ambapo alifunua poti lake hilo lenye chakula baada ya Yanga kufunga bao la pili.
*********************************************
TIMU ya Yanga SC jana ilirejea kileleni mwa Ligi Kuu Bara, baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Amissi Tambwe aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 70 na kumtengenezea Obrey Chirwa bao la pili katika dakika ya 74.
Kwa ushindi huo sasa Yanga wamefikisha jumla ya pointi 59 baada ya kucheza mechi 26 huku wakiwa na pointi sawa na Simba iliyocheza mechi 27, wakiwa na tofauti ya mabao. 
Katika mchezo huo uliomalizika dakika 45 za kipindi cha kwanza kwa sare ya 0-0, Kocha Mzambia, George Lwandamina, alifanya mabadiliko yaliyozaa matunda kwa timu yake kwa kuwatoa Hassan Kessy na kuingia, Juma Abdul na kiungo Haruna Niyonzima kwenda kuchukua nafasi kiungo Said Juma ‘Makapu’ kipindi cha pili.
Yanga ikabadilisha mipango ya kuishambulia ngome ya Prisons na kuanza kucheza gonga nyingi katikati ya uwanja.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.