Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA YANGA vs MBEYA CITY JANA

 Mabekiwa Yanga Hassan Kessy (kushoto) na Nadir Haroub, wakishangilia kwa furaha baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho katika mchezo wao dhidi ya Mbeya City, jana ambapo Yanga waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 na kurudi kileleni mwa ligi wakiwashusha mahasimu wao Simba kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku pointi wakiwa sawa.
**********************************************
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Dar Young Africans, jana wamekaa tena kileleni mwa Ligi hiyo baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo mabingwa hao watetezi sasa wamefikisha pointi 65 wakicheza mechi 28 wakibakiza mechi mbili mkononi na kuongoza Ligi hiyo.
Mahasimu wao Simba wamerudi nafasi ya pili huku wao pia wakiwa na pointi zake 65 na mechi 29, wakibakiza mechi moja mkononi.
Bao la Yanga lilifungwa na winga Simon Msuva kwa kichwa dakika ya saba tu akimalizia krosi ya Hassan Kessy.
Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (kulia) akichuana kuwania mpira nabeki wa Mbey City, Tumba Lui.
***********************************************
Baada tu ya Msuva kufunga bao hilo, hakuweza kushangilia bao lake wala kuendelea na mchezo, kutokana na kuumia na kupasuka paji la uso juu ya jicho la kulia alipogongana na beki wa Mbeya City, Tumba Lui na nafasi yake ikichukuliwa na beki Juma Abdul.
Kwa mabadiliko hayo, Kessy alikwenda kucheza kama winga wa kulia juu ya Abdul Abdul huku wakipokezana kuzuia na kushambulia. 
Kipindi cha pili Mbeya City walikianza vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Betram Nchimbi. dakika ya 57 akitumia mwanya wa mabeki wa Yanga kupoteana.
 Kessy akimkalisha Mwasapile
*********************************************
Yanga walipata bao la pili lililofungwa na mshambuliaji, Obrey Chirwa dakika ya 64 akimalizia mpira wa adhabu wa Juma Abdul.
Mrisho Ngassa aliingia kipindi cha pili upande wa Mbeya City, lakini hakuwa na madhara kwa timu ya yake ya zamani zaidi tu ya kusisimua mashabiki kwa uchezaji wake wa kuranda pande zote za uwanja. 
KIKOSI CHA YANGA: Benno Kakolanya, Hassan Kessy/Emmanuel Martin dk, Mwinyi Hajji Mngwali, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Kevin Yondan dk67, Thabani Kamusoko, Simon Msuva/Juma Abdul dk12, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya.
KIKOSI CHA MBEYA CITY: Owen Chaima, Haruna Shamte, Hassan Mwasapili, Tumba Lui, Sankani Mkandawile, Kenny Ally, Ditram Nchimbi, Majaliwa Shaaban, Zahor Pazi/Bryson Raphael dk46, Raphael Daudi na Rajab Isihaka/Mrisho Ngassa dk58. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
 Chirwa (Kulia) akichuana na Tumba
 Chirwa akishangilia bao lake huku akipongezwa na Emmanuel Martin
  Chirwa akimtoka beki wa Mbeya City, Hassan Mwasapile.
 Hassan Kessy akimtoka Mwasapile....
 Hassan Kessy akimtoka Majaliwa Shaban
 Hassan Kessy akiwatoka mabeki wa Mbeya City
 Kessy akipiga krosi
Kipa wa Mbeya City, Owen Chaima, akiruka kujaribu kupangua mpira uliopigwa kwa kichwa na Amis Tambwe na mshinda baada ya kugonga mwamba.
 Shabiki wa Yanga akishangilia kwa staili ya kuonyesha Kipolo
 Mashabiki wa Yanga wakilaumu baadhi ya matukio ya uwanjani
 Simon Msuva akimramba chenga beki wa Mbeya City, Sankani Mkandawile
 Msuva akiwania mpira na Lui
 Msuva akiwatoka mabeki wa Mbeya City
 Msuva akiwatoka mabeki wa Mbeya City
 Geofrey Mwashiuya (kulia) akichuana na Rajab Isihaka
 Haji Mwinyi (kulia) akichuana na Rajab Isihaka
 Mrisho Ngassa akimiliki mpira 
 Niyonzima akimtoka beki wa Mbeya City
 Niyonzima akipiga krosi
Amis Tambwe akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Mbeya City

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.