Habari za Punde

MECHI ZOTE ZA MWISHO LIGI KUU BARA KUANZA SAA 10.00 JIONI KESHO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tunafahamisha kuwa mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Muda huo umepangwa ili kuhakikisha timu zote zinamaliza mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinamalizika siku moja ya Mei 20, mwaka huu na kwa muda mmoja, ikiwa ni pamoja na kudhibiti viashiria vyo vyote vya upangaji wa matokeo.
Ni jukumu la kila kamishna kuhakikisha mechi anayosimamia inaanza katika muda ulipangwa bila kujali kama kuna mgeni rasmi au la.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.