Habari za Punde

MIILI YA WANAFUNZI 33, WALIMU WAWILI NA DEREVA YAAGWA JIJINI ARUSHA

Sehemu ya Jeneza zenye miili ya Wanafunzi 32, Walimu wawili na Dereva waliopoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Rhotia Wilayani Karatu hivi karibuni, zikiwa Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid wakati wa zoezi la kuaga lililoongozwa na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan. 
Umati wa wakazi wa Jiji la Arusha na maeneo ya jirani ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid wakati wa zoezi la kuaga miili ya Wanafunzi 32 wa Shule ya Sekondari ya Lucky Vicent, Walimu wao wawili na Dereva waliopoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Rhotia Wilayani Karatu hivi karibuni. Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan ndie aliongonza zoezi hilo la kuaga.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha wakishiriki kuaga miili ya wanafunzi hao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.