Habari za Punde

MISS TANZANIA 2016 HATIMAYE LEO AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA GARI

Mwakilishi wa  Baraza la Sanaa la Tanzania (Basata), Augustino Makame akikabidhi funguo ya gari kwa Miss Tanzania 2016, Diana Edward Lukumay jana.  Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Grace Products ltd, Elizabeth Kilili na Meneja Masoko wa  Duka la Jewellers Mohamed Hassan Salum.
*****************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Hatimaye Miss Tanzania, Diana Edward Lukumay amekabidhiwa zawadi yake ya gari baada ya kusubiria tokea mwezi Oktoba mwaka jana.
Kampuni ya Lino International Agency  ilishindwa kukabidhi zawadi ya gari kwa wakati   baada ya mdhamini wa kwanza aliyeahidi kutoa zawadi hiyo kujitoa hatua za mwisho baada ya shindano hilo kuhamia Mwanza.
Hatua ya kukabidhiwa zawadi mrembo huyo imetokana na agizo la serikali wa Kampuni ya Lino International Agency kukabidhi zawadi za warembo walioshiriki katika mashindano ya mwaka jana ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Kutokana na agizo hilo, kampuni ya Lino International Agency ilianza upya juhudi za kutafuta zawadi kwa mrembo huyo na kuzipata kampuni mbili, kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa  vipodozi asilia, Grace Product Ltd na duka la kuuza vito ;a  Gift Jewellers ambapo kwa pamoja waliamua kununua gari aina ya Suzuki Swift yenye thamani ya Sh milioni 9.
Mbali ya kununua zawadi hiyo, kampuni hizo pia zililifanikisha usajili wa gari hiyo na kupewa namba ya usajiliwa,T625DKL.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Diana aiwataka warembo wanaoshiriki katika mashindano ya Miss Tanzania kuwa wavumilivu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za mashindano hayo zinazotokana na matatizo ya kiuchumi.
“Nimefurahi  sana kukabidhiwa gari langu, nimeisubiri kwa muda mrefu na unatakiwa kywa mvumilivu ili kuendelea kuwa na nidhamu, na sasa kwa kupitia gari langu, nitafanya kampeni yangu ya kupiga vita mimba za utotoni na unyanyasaji kwa wanawake kupitia kampuni yake aliyoisajili,” alisema Diana.
Mrembo huyo pia aliwaomba warembo wajitokeza kushiriki katika mashindano  ya hayo pamoja na matatizo yaliyowakumba wao.
“Mashindano mazuri sana yenye kujenga mtu na kumpatia kipato, tokea nimalize mashindano, nimeweza kupata dili mbalimbali ambazo sikutaka kuziweka wazi kwenye jamii, zimekuwa ni shughuli zangu za kila siku,” alisema.
Mkuu wa Itifaki wa Kampuni ya Lino, Albert Makoye aliwashukuru wadhamini wao na kwa sasa wanaanza pilika pilika za mashindano ya mwaka huu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Grace Products ltd, Elizabeth Kilili alisema kuwa ameamua kudhamini zawadi ya gari kutokana na kuvutiwa na mashindano na hasa Diana ambaye anatumia vipodozi vya asili.
Mhasibu Mkuu wa duka la Gift Jewellers, Faudhia Salum alisema kuwa wamemua kuwezesha zawadi ya gari hiyo, kama moja ya shughuli zao za kijamii. Salum alisema kuwa wao kama wauzaji wa vito wamefarijika sana kusaidia mashindano hayo na hasa ukizingatia kuwa vito vingi uvaliwa na akina dada kwa lengo la kupendeza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.