Habari za Punde

PSPF YADHAMINI MAHAFALI YA PILI YA TAIFA YA WAHITIMU WA ELIMU YA JUU WALIOFANYA VIZURI KWENYE VITIVO VYAO

Muhitimu wa elimu ya juu, akisoma kipeperushi chenye maelezo ya shughuli zifanywazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa mahafali ya pili ya kitaifa ya wahitimu wa elimu ya juu waliofanya vizuri kwenye vitivo vyao mwaka 2016.Mahafali hayo yaliyowaleta pamoja zaidi ya wahitimu 100 yalidhaminiwa na Mfuko huo na kufanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Mei 19, 2017
Baadhi ya wahitimu hao wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mahafali.
Bw. Chacha Nyaikwabe, Meneja Kumbukumbu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wa PSPF kwenye mahafali hayo. Bw. Chacha alisema, PSPF imeamua kudhamini mahafali hayo kwa vile inajua fika, wahitimu hao ni watu muhimu wa kujiunga na Mfuko huo na kwa hali hiyo Mfuko umepata fursa ya kuwaeleza shughuli mbalimbali zifanywazo na PSPF ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama na Mafao yatolewayo na Mfuko huo kwa Mwanachama.
Rais wa TAHILISO, akizungumza kwenye mahafali hayo. Mahafali hayo yameratibiwa na TAHILISO. Kulia ni mgeni rasmi, 
Margareth Komba, Naibu Mkurugenzi Elimu ya Juu Sayansi na Ubunifu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na kushoto ni mwakilishi kutoka PSPF, Bw.Nyaikwabe.
Mgeni rasmi Bi. Margareth Komba, Naibu Mkurugenzi Elimu ya Juu Sayansi na Ubunifu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wakifurahia hotuba
Wahitimu wakisikilzia kwa makini kilichokuwa kikiendelea
Muhitimu akisoma kipeperushi chenye maelezo ya shughuli zifanywazo na PSPF 
Hawa ni baadhi ya vijana wa shule za sekondari ambao nao walifanya vizuri kwenye mitihani yao wakiimba wimbo wa taifa. Vijana hawa walialikwa ili kujipatia uzoefu kutoka kwa wahitimu hao wa elimu ya juu waliofanya vema kwenye vitivo vyao.
Wahitimu wakiwa kwenye matembezi ya mahafali ya kitaifa ya pili ya wahitimu wa elimu ya juu chini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.