Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP) SIMON SIRRO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha vyeo vipya Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro kabla ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha vyeo vipya Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro kabla ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akisaini Hati ya Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro mara baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
*************************************************
*SIRRO ASISITIZA USHIRIKIANO KUONDOA UHALIFU
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amewasisitiza wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wahalifu waliopo katika maeneo yao jambo ambalo litapunguza au kuondoa kabisa uhalifu nchini.
IGP Sirro ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi la Tanzania.
Amesema kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao hivyo ni wajibu wa jeshi hilo kuhakikisha nchi nzima ina ulinzi wa kutosha utakaopelekea wananchi kuishi kwa amani na utulivu na kuwawezesha kufanya kazi zao bila kubugudhiwa.
“Uhalifu hauwezi kupungua kwa kutegemea Jeshi la Polisi pekee bali tunahitaji nguvu ya pamoja ili kushinda vita hiyo, ushirikiano wa wananchi unahitajika kwa kiasi kikubwa”,Alisema IGP Sirro.
Ameongeza kuwa kipaumbele cha kwanza katika utendaji wake kwenye  nafasi hiyo ni kupambana na uhalifu pamoja nidhamu ya watendaji kazi kwani bila nidhamu, kazi ya kupambana na wahalifu haiwezi kufanikiwa.
Aidha, amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Pwani ambao umekuwa na mauaji na uhalifu wa mara kwa mara kuwa atafanyia kazi changamoto zinazowakabili na  kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu.
Kwa upande mwingine, IGP Sirro amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika cheo hicho pia amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa ushirikiano wake wakati alipokuwa akitumikia cheo cha Kamishna wa Polisi wa Kanda maalum ya Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, IGP Sirro alishika nyadhifa mbali mbali zikiwemo za Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamanda wa kikosi cha operesheni maalum na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam.     
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba,IGP mpya Simon Sirro,  IGP wa zamani Ernest Mangu pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Magereza.
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro pamoja na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Majeshi ya Polisi na Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Majeshi ya Polisi na Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba mara baada ya tukio la uapisho wa IGP Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.