Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI AOMBOLEZA VIFO VYA WANAFUZI 32, WALIMU 2 NA DEREVA KATIKA AJALI YA LEO WILAYANI KARATU

Zoezi la uokoaji likiendelea.
*************************************************
Ajali iliyotokea leso asubuhi eneo la Rhotia Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, iliyohusisha Basi la wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Lucky ya jijini Arusha, bada ya kupoteza mwelekeo na kupindukia korongoni wakati wakiwa safarini kuelekea Karatu kufanya mitihani ya ujiranimwema na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini English Medium ya mjini Karatu. imeua jumla ya wanafunzo 32, walimu 2 na dereva 1.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alitaja idadi hiyo ya wanafunzi 32 , walimu 2 na dereva wa gari hilo kuwa walipoteza maisha papo hapo katika ajali hiyo  huku wanafunzi watu sita katika ajali hiyo wakijeruhiwa. 
Umati wananchi ukiwa katika nje ya chumba cha maiti cha hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kutambua miili ya wanafunzi na wanafunzi waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Umati wananchi ukiwa katika nje ya chumba cha maiti cha hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kutambua miili ya wanafunzi na wanafunzi waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.