Habari za Punde

RIADHA INA NAFASI KUBWA KATIKA KUTUUNGANISHA WANA AFRIKA MASHARIKI NA KATI : WAZIRI DKT MWAKYEMBE

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harisson Mwakyembe (wa kwanza kulia)  akimvalisha medali mshindi wa mchezo wa kurusha mikuki Bi Mwanaamina Hassan kutoka Tanzania katika mashindano ya Riadha kwa vijana walio chini ya miaka 18 yaliyoshirikisha nchi saba za Afrika Mashariki na Kati  leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harisson Mwakyembe (katikati) akizungumza  leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anafungua mashindano ya Riadha kwa vijana walio chini ya miaka 18 yaliyoshirikisha nchi saba za Afrika Mashariki na Kati yanayofanyika kwa siku mbili katika Uwanja wa Taifa Dar es Salam Tanzania ikiwa ndio mwenyeji wa mashindano hayo.Kushoto ni Mkamu wa Chama cha Riadha Tanzania Dkt. Hamad Ndee.
 Mshiriki wa Riadha kwa vijana walio chini ya miaka 18 yaliyoshirikisha nchi saba za Afrika Mashariki na Kati Bi Keflin Kipili kutoka Tanzania   akila kiapo cha utii kabla ya kuanza mashindano hay oleo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harisson Mwakyembe (wa kwanza kulia)  akimvalisha medali mshindi wa mchezo wa kurusha mikuki Bw. Najim Ally  kutoka Zanzibar katika mashindano ya Riadha kwa vijana walio chini ya miaka 18 yaliyoshirikisha nchi saba za Afrika Mashariki na Kati  leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Nchi zilizoshiriki mashindano ya Riadha kwa vijana walio chini ya miaka 18 yaliyoshirikisha nchi saba za Afrika Mashariki na Kati yanayofanyika kwa siku mbili katika Uwanja wa Taifa Dar es Salam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harisson Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Riadha na Washindi wa mashindano ya Riadha kwa vijana walio chini ya miaka 18 yaliyoshirikisha nchi saba za Afrika Mashariki na Kati leo Jijini Dar es Salaam.
*************************************************
Na Shamimu Nyaki - WHUSM
Mchezo wa Riadha umekuwa na mchango   mkubwa katika kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya Afrika Mashariki na Kati kwa kuwa  nchi wanachama wamekuwa wakifanya mashindano mbalimbali yaliyochangia kuleta ukaribu miongoni mwa Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa   leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akifungua mashindano ya Riadha kwa vijana wenye umri chini ya Miaka 18 yaliyojumuisha nchi saba za Afika Mashariki na Kati ambapo ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha vijana wenye vipaji na uwezo wa kufanya riadha kutumia mashindano hayo kama njia ya kujifunza na kufanya vizuri.
“Mashindano haya ni mazuri yanatoa  hamasa kwenu vijana kuyatumia kama njia ya kujifunza ili mfanye vizuri kama wanariadha wengine waliowahi kufanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Afrika lakini pia yametuunganisha sisi wana Afrika Mashariki na Kati pamoja na kuimarisha uhusiano wetu ”Alisema Mhe. Waziri.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania   Bw. Filbert Bayi ameeleza kuwa mchezo wa riadha umeanza kurudi katika hadhi yake ya zamani baada ya vijana wengi kuanza kuupenda na kushiriki mashindano mbalimbali ya riadha  ambayo yamekuwa yakiwapatia mafanikio.
“Hivi sasa riadha imeanza kupendwa vijana wengi wanajitokeza katika mchezo huu na   mashindano mbalimbali wakiwa na ari kubwa ya kutamani kufika mbali tunachotakiwa kufanya ni kuwaunga mkono,” Aliongeza   Bw Filbert.
Naye Mshiriki wa Mshindi wa Mita 100 kutoka Tanzania Bi Keflin Kipili amesema kuwa riadha ni mchezo unaoleta mafaniko hivi sasa Ulimwenguni kwa vijana kama yeye hivyo ni vyema kwa vijana kuumia vipaji walivyonavyo anatumia kupata mafanikio zaidi.
Katika mashindano hayo Nchi ya Kenya imekuwa kinara kwa kuibuka kidedea kwa kushinda medali tatu za dhahabu katika mbio za mita 800 Wasichana na Wavulana,pamoja na mita 3000 Wavulana huku Tanzania ikiibuka kidedea katika mbio za mita 100 Wasichana, kubadilishana vijiti (relay) Wasichana na Wavulana.

Mashindano hayo ya siku mbili yanafanyika Jijini Dar es Salaam yanahusisha Nchi   saba za Afrika mashariki na Kati ambazo ni Tanzania ambao ndio wenyeji, Kenya,Zanzibar,Somalia,Sudan Kusini na Eritrea.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.