Habari za Punde

SERENGETI BOYS OUT MICHUANO YA VIJANA AFRIKA, NIGER YASONGA


TIMU ya Vijana ya Tanzania, Serengeti Boys, imefungwa bao 1-0 na Niger na kuondolewa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, katika mchezo wa mwisho wa Kundi B usiku wa jana katika Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, Gabon.
Kwa matokeo hayo yanaisongesha timu ya Niger baada ya kufungana kwa pointi na Tanzania na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, ambapo kwa kanuni mshindi katika mchezo huo moja kwa moja anafuzu michuano ya Kombe la Dunia inayotarajia kuwanza mwezi Oktoba mwaka huu nchini India na pia kushiriki Nusu Fainali ya michuano hiyo.
Niger anaungana na Mali iliyoongoza kundi ikiwa na pointi saba, baada ya ushindi wa mechi mbili na sare moja, wakati Tanzania na Angola zote zikiaga michuano hiyo.
Katika mchezo huo timu ya Niger ilipata bao katika dakika ya 41 kipindi cha kwanza, likifungwa na Ibrahim Boubacar Marou, baada ya kipa na mabeki wa Serengeti Boys kujichanganya langoni huku aliyepiga mpira huo akionekana kuwa nje ya uwanja na kuurudisha mipra wa juu ndani na kumgonga beki na kisha kujaa wavuni.
Lakini Niger wangetoka uwanjani wanaongoza kwa mabao zaidi baada ya dakika 45 kama za kipindi cha kwanza kama si umahiri wa kipa Ramadhan Kabwili, kuokoa michomo zaidi ya mitatu ya wazi.
Kwa ujumla, Serengeti Boys ilizidiwa mchezo kipindi cha kwanza na kipindi cha pili hali iliendelea kuwa hivyo.
 Wachezaji wa Tanzania walikuwa wenye huzuni baada ya mchezo huku wakilia. 
Mbali na Mali na Niger, timu nyingine zilizofuzu Nusu Fainali ni Ghana na Guinea kutoka Kundi A. 
 
 KIKOSI CHA TANZANIA: Ramadhani Kabwili, Ally Ng'anzi, Nickson Kibabage, Dickson Job, Abdul Suleiman, Asad Ali/Muhsin Makame dk85, Kibwana Ally, Shaaban Zuberi, Ally Msengi, Ibrahim Abdallah/Yohanna Nkomola dk46 na Kelvin Naftal.
KIKOSI CHA NIGER: Khaled Ibrahim, Yacine Massamba, Habibou Sofiane, Rachid Souley, Abdoul Karim, Djibrilla Ibrahim, Inoussa Amadou, Abdoul Rachid, Ibrahim Boubacar, Ibrahim Namata na Hamid Galissoune Ajina.
Kipa wa Serengeti Boys, Ramadhan Kabwili
 
akilia huku akifarijiwa na wenzake baada ya mchezo huo kumalizika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.