Habari za Punde

SERENGETI BOYS YAJIWEKA PAZURI KUELEKEA KOMBE LA DUNIA,YAICHAPA ANGOLA 2-1

TIMU ya Viaja wa tanzania serengeti Boys, ni kama imetanguliza mguu mmoja Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 17 Oktoba mwaka nchini India, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angola na kufikisha pointi Nne katika mchezo wa Kundi B Fainali za U-17 Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa L’Amittee mjini Libreville, Gabon.
Kwa ushindi huo Serengeti Boys inaongoza Kundi B, baada ya kucheza mechi mbili, ya kwanza ikitoa sare ya 0-0 na Mali katika mchezo uliopigwa mwanzoni mwa wiki hii.
Tanzania walitangulia kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake tegemeo Yohana Mkomola, katika dakika ya tano kwa kichwa akiunganisha krosi ya Enrick Nkosi, kabla ya Francisco Chilumbo kuisawazishia Angola dakika ya 19.
Serengeti Boys ingeweza kumaliza kipindi cha kwanza inaongoza kwa mabao zaidi, kama wachezaji wake wangekuwa makini katika kutumia nafasi walizotengeneza.
Kipindi cha pili, nyota ya Serengeti Boys iliendelea kung’ara, lakini tatizo likabaki kuwa umalizijia wa nafasi walizokuwa wakitengeneza.
Hata hivyo, Abdul Suleiman awapa raha Watanzania kwa kufunga bao zuri la ushindi dakika ya 69 akimalizia pasi ya Yohanna Oscar Nkomola.
Angalau pasi ya bao aliyotoa mwa Abdul itamfariji Nkomola, kwani ndiye mchezaji aliyepoteza nafasi nyingi za mabao leo. 
Serengeti Boys itashuka tena dimbani Mei 21 kucheza mechi yake ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Niger, ambayo leo inamenyana na mabingwa watetezi, Mali. Timu zitakazoingia Nusu Fainali zitafuzu moja kwa moja fainali za Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.