Habari za Punde

SERIKALI YAANZISHA KIKOSI KAZI CHA KUDHIBITI UHALIFU WA JINAI KATIKA TASNIA YA MISITU NA WANYAMAPORI.


Na Nuru Juma, Husna Saidi, 
MAELEZO.
SERIKALI imeanzisha kikosi kazi cha kudhibiti uhalifu wa kijinai katika tasnia ya misitu na wanyamapori ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya wanyamapori na mazao ya misitu wa mwaka 2014-19.
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi jana Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema kikosi kazi hicho kinatumia teknolojia ya ndege maalum zisizo na rubani na mbwa maalum kwa ajili ya kukabili ujangili na biashara haramu ya nyara za Serikali.

Anaongeza kuwa hadi sasa Wizara iliendesha jumla ya siku-doria 349,102 ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa na kuwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 7,085 na meno ya tembo 129 na vipande vya meno 95 vyenye uzito wa jumla ya kilo 810.03.

Profesa Maghembe anaongeza kuwa Wizara yake pia ilifanikiwa kukamata silaha za kivita 48, silaha za kiraia 150, risasi 1,058, magobore 406, silaha za jadi 22,307,roda 120,538 pamoja na pikipiki 189, baiskeli 214, magari 20, ng’ombe 79,831 na samaki kilo 4,043.
“Kupitia doria hizo jumla ya kesi 2,097 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali h nchini, jumla ya kesi 802 zilikamilika ambapo kesi 262 zenye watuhumiwa 472 walifungwa jela ya miezi 42,153” alisema Profesa Maghembe.

Akifafanua zaidi Profesa Maghembe alisema kesi nyingine 43 zenye watuhumiwa 79 zilikamilika kwa wahusika kuachiwa huru wakati kesi 276 zenye watuhumiwa 469 walilipa faini jumla ya Tsh. Milioni 452 na kesi 966 bado zinaendelea.

Kuhusu mfuko wa wanyamapori, Prof. Maghembe anasema katika mwaka 2016-17 mfuko umetumia Tsh Bilioni 6.7 kuwezesha utekelezaji wa kazi za kuhifadhi na miradi ya maendeleo zikiwemo doria na kukiwezesha kikosi kazi maalum cha kupambana na ujangili

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.