Habari za Punde

SIMBA MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA FA WAICHAPA MBAO FC 2-1

TIMU ya Simba SC imejiwekea uhakika wa kupanda ndege mwakani baada ya leo kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho ambapo watashiriki Kombe la Shirikisho hapo mwakani wakiifunga Mbao Fc mabao 2-1 katika mchezo wa faina za FA katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jioni hii.
Katika mchezo huo Simba walitangulia kupata bao katika dakika za nyongeza baada ya kumalizika dakika 90 bila kufungana na katika dakika 15 za kwanza Simba walipata bao ambalo halikudumu kwani dakika chache baadaye Mbao Fc walisawazisha na dakika 15 zapili Mbao walipata tena bao ambalo lilikataliwa na dakika chache tena Simba walipata kona iliyozaa penati ambayo ilipigwa na Shiza Kichuya na kuwapa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.