Habari za Punde

SIMBA WAIPIGISHA DEBE STAND UTD UWANJA WA TAIFA 2-1 NA KUREJEA KILELENI

Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo (kushoto) akichuana na beki wa Stand Utd, Ibrahim Job, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Juma Luizio katika dakika ya 23 na 35 kipindi cha kwanza, huku Stand Utd wakiwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Suleiman Kassim 'Selembe' katika sekunde ya 58 tu baada ya kuanza kwa mtanange huo.KWA ushindi huo wa leo Simba wanafikisha pointi 65 wakiwa tayari wamecheza mechi 29, wakibakiza mchezo mmoja wakiwa na zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 62, ambao wanaweza kukaa kileleni kwa mabao zaidi, wakiifunga Mbeya City katika mchezo wao wa kesho Uwanja wa Taifa.
Hapa ilikuwa ni shughulia pevu kati ya Job na Mavugo.
Bao la pili la Simba lililozua kizazaa kwa wachezaji wa Stand kumzonga mwamuzi wakimlaumu kuwa aliyepiga krosi hiyo, Shiza Kichuya (pichani kushoto) alikuwa ameotea.
Wachezaji wa Stand Utd wakimzonga mwamuzi wa mchezo huo baada ya bao la pili wakidai kuwa lilikuwa ni la kuotea.
Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo (katikati) akipiga shuti katikati ya mabeki wa Stand Utd, waka ti wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mavugo akikosza bao dakika za mwisho.
Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo akichuana kuwania mpira na beki wa Stand Utd, Ibrahim Job, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mohamed Ibrahi wa Simba (kushoto) akimhadaa beki wa Stand Utd, Erick Mulilo, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
KIKOSI CHA SIMBA SC: Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, James Kotei, Shiza Kichuya/Abdi Banda dk78, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Juma Luizio/Pastory Athanas dk61, Jonas Mkude na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Mwinyi Kazimoto dk51.
KIKOSI CHA STAND UTD: Frank Muwonge, Aaron Lulambo/Rajab Rashid dk81, Jacob Massawe, Miraj Maka, Revocatus Richard, Erick Mulilo, Adam Salamba, Kheri Khalifa/Sixtus Sabilo dk70, Frank Khamis, Ibrahim Job na Suleiman Kassim ‘Selembe’.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.