Habari za Punde

SIMBA WAJIPANGA KUISHITAKI KAMATI YA KATIBA NA SHERIA, TFF FIFA

WAKATI Uongozi wa Klabu ya Simba ukisubiri kupewa barua ya kuthibitisha kupokwa Pointi tatu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Kagera Sugar, sasa Uongozi huo umesema kuwa wamepanga kwenda kushitaki katika Mahakama ya usuluhishi ya FIFA (CAS) mara tu baada ya kupokea barua hiyo.
Simba ilipoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 2-1, na baadaye kupewa pointi tatu baada kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi (Kamati ya saa 72) kujiridhisha kuwa Kagera walimchezesha beki Mohamed Fakih ambaye alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo huo pointi ambazo baadae zilirejeshwa kwa Kagera na kamati hiyo hiyo ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rais wa klabu hiyo Evans Aveva, alisema kama Uongozi hawawezi kukubali kuona timu yao inaonewa tena na TFF na na kusema hivi sasa wanasubiri kukabidhiwa barua ya kuporwa pointi tatu hizo ili wapeleke malalamiko yao CAS.
“Tumeonewa mara nyingi, mfano suala la wachezaji Mbaraka Yusuph, Hassan Kessy na Ramadhan Singano ‘Messi’ walikuwa wachezaji wetu halali lakini TFF wakawaidhinisha kucheza timu nyingine, huu ni uonevu tumechoka kuonewa tunaenda FIFA,” alisema Aveva.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 59 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56 na michezo miwili mkononi ambayo ikishinda yote itaizidi Simba kwa pointi tatu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.