Habari za Punde

SIMBA YACHUKUA BANDO LAKE LA SIKU KWA YANGA YAICHAPA AFRICAN LYON 2-1

 Kikosi cha Simba
********************************* 
TIMU ya Simba SC leo imerejea kileleni baada ya kuichapa African Lyon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo Simba sasa wamefikisha jumla ya pointi 62 huku mahasimu wao Yanga wakiwa na pointi 59. Mabao ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza na bao la pili Beki Hamadi Waziri akijifunga katika kipindi cha pili.
Beki  wa Simba, Janvier Bukungu (kushoto) akichuana kuwania mpira na Omary Abdallah, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, 
Beki  wa African Lyon, Miraj Adam,  akiruka kuokoa mpira huku akizongwa na Mohamed Ibrahim, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
KWA MATUKIO ZAIDI YA MTANANGE HUU KAA NASI HAPPO BAADAYE

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.