Habari za Punde

SINGIDAUNITED YAENDELEA KUWASHIKA YAMSAINISHA KENNY ALLY WA MBEYA CITY

Kiungo mchezeshaji wa timu ya Mbeya City, Kenny Ally (katikati) akisaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya Singida United wakati wa hafla hiyo fupi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahman Sima na Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Singida Festo Sanga.
***********************************
Kenny Ally Kiungo wa Mbeya City, aliyekuwa akiwindwa na Vilabu vikubwa vya Yanga na Simba, hatimaye amesaini mkataba wa miaka miwili na timu iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao Singida Utd  kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Mbeya City tangu walipopanda Ligi Kuu wamekuwa wakiporwa wachezaji wao wanaoonekana kufanya vizuri na kuacha pengo katika timu hiyo, ambapo kwa mara nyingine tena usajili kiungo huyo kwenda Singida United ni pigo kwa timu yake Mbeya City.
Singida United ni miongoni mwa timu ambazo zimeanza kutazamwa na wadau wa soka kutokana na usajili wake unaoendelea  na kuwafanya wadau wa soka kuamini kuwa huenda timu hiyo ikaleta upinzani kwa timu wenyeji katika Ligi Kuu Bara msimu ujao 
Mchezaji Kenny Ally akipokea jezi yake namba nane kutoka kwa Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahman Sima baada ya kusaini mkataba wake.Katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Singida Festo Sanga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.