Habari za Punde

SPIKA WA BUNGE AKABIDHI KIKOMBE MECHI YA BUNGE NA NMB

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (Kushoto)akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge, Mheshimiwa Sixtus Mapunda mara baada ya mechi kuisha na timu ya Bunge kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa bila dhidi ya NMB,  mechi hiyo ilifanyika jana katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na  Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (Kulia) ambae pia ni mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Bunge kabla ya kuanza mechi ya mpira wa pete kati ya Timu ya Bunge na Timu ya NMB iliyofanyika jana katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Wachezaji wa timu ya Mpira wa pete wa Bunge na NMB wakipiga picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mechi yao ambayo ilifanyika jana katika uwanja wa jamhuri Mjini Dodoma. PICHA NA OFISI YA BUNGE

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.